DAR ES SALAAM: Leo Desemba 9 Tanzania Bara imeazimisha miaka 55 tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa wakoloni mwaka 1961.
Maadhimisho hayo yamepambwa na
shughuli mbalimbali za kijeshi lakini pia ngoma za asili kutoka kwa
makundi mbalimbali pamoja na Rais Magufuli ambaye pia ni Amri Jeshi Mkuu
kukagua Gwaride la uhuru, sherehe ambazo kitaifa zimeashimishwa kwenye
Uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam.
Mbali na mambo hayo yaliyoonekana
kuwavutia wengi, jambo lingine lililowafurahisha ni pale Rais Dk
Magufuli alipoamua kutembea kiukakamavu kama mwanajeshi mara baada ya
kumaliza kukagua gwaride katika maadhimisho haya ya 55 ya uhuru.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment