MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Nipe namba ya mumeo”
“Eehee”
“Nipe namba ya mumeo, hujanisikia?”
Phidaya
kwa uwoga akaichukua simi yake aliyo kua ameiweka pembeni ya glasi
iliyo jaa juisi ya embe, vyote kwa pamoja vikiwa juu ya meza ya kioo
iliyopo ndani ya kibanda hicho. Kwa kutetemeka Phidaya akaitafuta namba
ya simu ya mumewe na kumuonyesha Mzee Godwin, ambaye taratibu akainadika
kwenye simu yake na kuipiga namba
hiyo.
ENDELEA
“Mwanangu Phidaya”
Mzee
Godwin alijibu kwa kujiamni, jambo lililo zidi kumchanganya Eddy ambaye
mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio, kwani uhasama wake na Mzee
Godwin ni mkubwa kupita kiasi.
“Nakuomba usifanye chochote kwa mke wangu, nakuomba baba yangu”
“Mmmm leo ndio unajua kwamba mimi ni baba yako?”
Mzee
Godwin aliendelea kuzungumza kwa dharau jambo lililo zidi kumpagawisha
Eddy, kwani umbali kutoka Dododma hadi Dar es Salaam, unachukua muda
mwingi sana kuweza kufika mbaya zaidi bado anakipengele cha kumalizia
bungeni kuweza kujibu maswali atakayo ulizwa kama waziri wa ulinzi,
ambaye amechukua majukumu ya kusimamia sekta zote za jeshi kuanzia
polisi hadi jeshhi la kujenga taifa, na wizara ya mambo ya ndani
ikatolewa katika usimamizi wa jeshi la polisi na kubaki ikiendelea
kusimamia mabo mengi na si jeshi la polisi, ambalo lilihamishiwa kwenye
wizara ya ulinzi moja kwa moja
“Leo, mke wangu atanipikia chakula kizuriii, kwahiyo usiwe na wasiwasi wowote, wewe endelea kupiga kazi”
Baada
ya kuzungumza hivyo mzee Godwin akakata simu, na kuizima kabiasa kisha
akamtazama Phidaya ambaye bado anaendelea kutetemeka mwili wake wote kwa
woga mwingi ulio mtawala. Madam Mery akatoa kitambaa cheupe kilicho
kunywa vizuri ambacho walikipulizia madawa ya kulevya kisha akamkabidhi
mzee Godwin.
Mzee
Godwin akamsogelea Phidaya sehemu alipo na kumziba na kitambaa hicho
puani mwake, Phidaya akajitahidi kushindana nguvu na mkono wa mzee
Godwin ulio mziba puani ila akajikuta akishindwa, huku nguvu zikianza
kumuishia taratibu taratibu hadi akalala fofofo.
Mzee
Godwin akambeba Phidaya begani na kuingia naye ndani, ambapo wakamlaza
kwenye moja ya sofa kubwa walilo likuta hapo sebleni, kisha akaanza
kuingia chumba kimoja baada ya kingine kuweza kutafuta funguo ya gari
walizo zikuta zimewekwa sehemu maalu za maegesho. Madam Mery yeye akawa
na kazi ya kuchungulia madirishani ili kuweza kuona nje kama kuna mtu
anaingia aweze kumstua mzee Godwin ambaye anaendelea kuwajibika na
utafutaji wa funguo hizo.
Mngurumo
wa gari, ukisimama nje, ukamstua Madama Mery aliye kuwa ameketi kwenye
sofa, kila mara akitazama tazama saa yake ya mkononi, akihesabu muda
jinsi unavyo kwenda. Akasimama kwa haraka na kwenda kuchungulia
dirishani, akamuona mtoto mdogo wa kiume akishuka kwenye gari hilo aina
ya BMW Z8, huku akiwa ameongozana na mtu anaye onekana kama ni dereva.
Kwa
jinsi mototo huyo anavyo fanana na Eddy moja kwa moja Madam Mery
akagundua kwamba huyo ni mtoto wa Eddy. Kwa haraka Madam Mery
akapandisha ngazi za kuelekea gorofani, ambapo ndipo alipo Mzee Godwin.
Kwa bahati nzuri akakutana na Mzee Godwin akitoka kwenye moja ya chumba
akitaka kuelekea kwenye chumba kingine.
“Vipi?”
“Kuna watu wanakuja”
Madam Mery alizungumza huku akihema kwani, alizipandisha ngazi hizo zipatzo thelathini kwa kukimbia
“Kina nani?”
Mzee
Godwin alizungumza huku akitembea kuelekea sehemu ambapo ataweza kuiona
seble vizuri. Mzee Godwin akamshuhudia mjukuu wake Junio akiingia huku
nyuma akiwa ameongozana na dereva wa gari aliye mleta. Junio
akamkimbilia mama yake aliye lala kwenye sofa na kumrukia kwa lengo la
kumstua, ila hakufanikiwa kumstua mama yeka kwani hakuweza kustuka wala
kutikisika, jambo lililo mpa wasiwasi mwingi Junio na kumfanya anze
kulengwa lengwa namachozi.
***
Eddy akajaribu kuipiga tena namba ya Mzee Godwin iliyo toka kumpigia
muda mchache ulio pita ila haikupatiokana, wasiwasi mwingi ukazidi
kumsumbua Eddy, akajaribu kupiga kwa mara ya pili ila hali ikawa ni ile
ile ya kuto kupatikana kwa namba hiyo. Akajaribu kuipiga namba ya mke
wake, ikaita pasipo kupokelewa.
“Mungu wangu?”
Eddy
alizungumza huku akizunguka zunguka ndani ya chumba huku jasho jingi
likimwagika mwilini mwake, na kujikuta akifungua vifungo vyote vya shati
lake. Eddy akafungua mlango na kuanza kutembea kwenye kordo ndefu, ya
hoteli aliyo fikizia akielekea sehemu ya mapokezi, kabla hajafika
akakutana na askari wake anaye mlinda
“Vipi muheshimiwa”
“Nahitaji kwenda, Dar sasa hivi”
Eddy alizungumza kwa haraka huku akizidi kupiga hatua kuelekea nje ya hotel hiyo kwenda kwenye maegesho ya magari.
“Unakwenda kufanya nini muheshimiwa?”
“Mke
wangu ametekwa, fanya hivi mpigie simu naibu waziri, mkabidhi mafaili
yangu yote na kipindi cha pili yeye ndio atajibu maswali sawa”
“Sawa mkuu”
Eddy akafika kwenye gari lake, na kumkuta dereva akiwa amejilaza.
“Shuka nipishe niendeshe”
Eddy alizungumza na kumfanya dereva wake kustuka kutoka usingizini
“Mmmmm”
“Hujanisikia au, nimekuambia kwamba zunguka upende wapili wa gari, tunahitaji kwenda Dar es Salaam sasa hivi”
“Muheshimiwa ni jukumu langu mimi kukuendesha”
“Wewe mzee, mimi ni nani yako? Nimekuambia nipishe”
Eddy
alizungumza kwa hasira na kumfanya mzee Selemani Mbogo, kutii amri ya
bosi wake, akashuka kwa haraka na kuzunguka upende wapili wa gari,
askari akataka kuingia kwenye gari ila Eddy akamzuia
“Wewe baki, hakikisha document zangu zote unampa naibu waziri sawa?”
“Sawa mkuu”
“Naomba bastola yako”
Hapo
askari akasita kidogo kuichomoa bastola yake aliyo ichomeka kiunoni
mwake, kwa ishara Waziri Eddy akamuomba amkabidhi bastola hiyo, taratibu
askari huyo akaichomoa na kumpa bosi wake. Eddy akaipokea na kuifunga
mlango wa gari, akaliwasha, akakanyaga mafuta pamoja na breki na
kuzifanya tairi za gari hilo kuserereka, na kutoa moshi mwingi, kisha
akaachia breki na kulifanya gari hilo kuchoka kwa kasi, na kuwafanya
watu wlaiopo katika eneo la hoteli kushangaa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment