Dar
es Salaam. Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 5,678 ikiwa
ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira, wafungwa 1,340 wataachiwa huru na 4,338 watatumikia kifungo
kilichobaki baada ya kupunguziwa moja kwa sita ya vifungo vyao.
Rais ametoa msamaha huo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45 (1) (d) ya Katiba.
Rwegasira imeeleza kuwa wafungwa wote
wamepunguziwa vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa
chini ya kifungu 49(1) cha sheria ya Magereza sura ya 58.
Amesema wafungwa waliopewa msamaha huo
ni pamoja na wagonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu (TB) na saratani na ambao
wamethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa
Mkoa au wa Wilaya.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment