ILIPOISHIA
“Yule mshenzi amepewa uwaziri wa ulinzi Tanzania?”
“Mungu wangu………ana sifa gani za yeye kuwa waziri?”
“Ndio
hivyo. Yaani laiti ningejua huyu mchenzi ningemuua tangu tukiwa ndani
ya ndege ninaamini kwamba tusinge kuwa tunazungumza mazungumuzo ya
kumuuhusu huyu kibwengo mtu”
“Kwa nini usimuue?”
“Mazingira hayakuruhusu, alipelekea kunipa shida ya kutafutwa hapo bendeni kwa hayati Mzee Madiba”
“Ulitokaje tokaje ndani ya ndege?”
Swali
la Madam Mery likamfanya Mzee Godwin kurudisha kumbukumbu zake nyuma
kwa haraka hadi siku aliyo toka kupambana na Eddy ndani ya ndege na
taratibu akaanza kusimulia.
ENDELEA
“Nilipo
onekanana sura yangu, iliniazimu mimi kuondoka na kuachana na Edddy
kwani endepo ningeendelea kupambana naye ningeingia mikononi mwa askari
na ingekuwa ni swala jengine.”
“Nilijichanganya
katikati ya askari ambao walikuwa wakikagua watu basi, nikafanikiwa
kutoka pasipo wao kugundua kwamba mimi ndio niliye kuwa nimesababisha
maafa hayo”
“Sasa uliingiaje ndani ya ndege?”
“Ahaa, nilimtumia njia ya kujificha kwenye mizigo, baada ya kumuona Eddy akiwa anahangaikia usafiri wa kuja nchini Tanzania”
“Aiseee una hatari kweli kweli wewe”
“Weee
acha tu, sasa lengo na thumuni la kukuita hapa ninahitaji kuweza
kumpoteza Eddy mara moja kwenye huu uso wa dunia. Ila tahadhari ni moja,
dogo amekuwa waziri, tena waziri wa ulinzi”
“Kama nilishindwa kumuua kipindi akiwa mtu wa kawaida, basi ujue kazi ya kumuangamiza yeye ni kubwa sana”
Madam
Mery akashusha pumzi nyingi huku akimtazama Mzee Godwin anaye onekana
kuwa na mawazo mengi kichwani mwake. Mzee Gowin kabla hajaendelea
kuzungumza ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yake, taratibu akaanza
kuusoma, na tabasamu pana likajijenga usoni mwake ikiwa ni ishara ya
furaha
***
Kukamatwa kwa mchungaji Mandingo na Madam Glory watu maarufu katika
nchi ya Tanzania kukaana kuwashangaza wananchi wengi, vyombo vingi vya
habari vilidai kwamba watu hao wamekamatwa na waziri mpya wa ulinzi.
Waandishi wengi walifunga foleni kwenye jengo la waziri wa ulinzi
wakihitaji kufanya mkotano na waziri huyo ambaye hadi sasa hivi
hawamuelewi nini ni maana ya kuwakamata watumishi hao wenye kumsaidia
kila mwenye shida mbele ya macho yao
“Muhesimiwa, muheshimiwaa”
Waandishi baadhi walimuuita Eddy alipo kuwa akishuka kwenye gari lake.
“Ni kwa nini umeamua kuwakamata watumishi wa bwana Mchungaji Mandingo na Madam Grory?”
Muandishi mmoja wa gazeti la Habari Sasa alimuuliza waziri Eddy Godwin
“Siwezi kuzungumza lolote kwa sasa, ila huo ni mwanzo tu waujibikaji wangu, ila kazi inaendelea”
Eddy
alijibu na kuomba kupishwa kukiwahi kikao cha wakuu wa jeshi la polisi
ambao tayari wamesha wasili kwenye ukumbi wa mikutano tangu saa mbili
asubuhi. Eddy hakuwa na haja ya kwenda ofisisni kwake moja kwa moja
akaelekea katika ukumbi wa mkutano, Akawakuta wakuu wote wa jeshi la
polisi, kutoka mikoani mwote wakiwa wanamngojea.
“Wakubwa zangu shikamoni”
Waziri
Eddy alisalimia kwani watu wote waliomo ndani ya ofisi yake wamempita
umri mkubwa sana na wengine ni sawa na baba zake. Kila mmoja akaitikia
salamu hiyo
“Samahani kwa kuchelewa kuweza kuwahi kwenye kikao, ila hakuna kilicho haribika.”
“Lengo la kuwaita hapa ninahitaji kujadiliana nanyi, kuhusiana na watendaji wenu katika mikoa yenu.”
“Napenda
kujua ni nini kilicho pungua kwenye idara yenu kuanzia madai munayo
idaia serikali ili yaweze kulipwa haraka iwezekanavyo”
Eddy alizungumza na kuwatazama wakuu wote walio fika kwenye kikao hichi. Mmoja akanyoosha kidole na kuzungumza.
“Mkuu
hapo kinacho tusumbua kwanza ni ufinyu wa mishahara kwa vijana wetu,
mishahara kupungua na mazingira mabaya ya nyumba wanazo ishi kambini.
Magari ni machakavu, piklikipi za doria ni chache kwahiyo inapelekea
vitendo vingi vya uhalifu kufanyika katika nchi yetu”
“Asante nitalishuhulikia, mwengine”
“Muheshimiwa
sisi tunahitaji sihasa isiingizwe kwenye majeshi kama hawa wezako walio
pita kwa maana walikuwa wakituletea siaaa kwenye kazi zetu na kujikuta
vijana wetu wakishindwa kufanya kazi kwa amani, jambo linalo pelekea
uhalifu kuzidi kuongezeka”
“Asante
baba yangu, ngoja niwatoe hofu kwenye hili. Mimi si mwana siasa na wala
sina chama ila ninanchi. Labda nitoe rai moja kwenu. Musidanganyike na
mwanasiasa yoyote. Yoyote ambaye ataingia kwenye jeshi la polisi, kama
muhalifu hakikisheni munamuua na si kumuacha hai”
Wazo
la waziri Eddy Godwin likawafanya wakuu wengi wa jeshi kushangaa kwani
hawakutegemea kupata wazo kama hilo kwenye kikao hicho.
“Muheshimiwa
kumbuka kwamba sisi ni jeshi la polisi kazi yetu ni kulinda wananchi na
mali zao. Sasa unapo sema tuwaue inakuwa ni kazi kidogo kwetu huoni
kwamba tutakuwa na sifa mbaya?”
“Samahani
baba yangu kwa majibu haya nitakayo kupa, ila kiukweli hadi sasa hivi
nyinyi muna sifa mbaya mbaya mbaya zaidi ya shetani na ubaya wake.
Wahalifu wengi tupo nao huku juu serikalini. Wanawatumikisha vijana
wadogo wanakamatwa na kufungwa, ila muzizi ipo inaendelea kuzalisha
matatizo mengine mengi kwenye ngi hii. Sasa hii ni amri wala sio ombi,
na lolote litakalo fanyika basi mimi nitakuwa muwajibikaji katika
kuyajibu hayo ICC”
Baadhi ya wakuu wa polisi wakapiga makofi kwa ujasiri anao uonyesha kijana mdogo mwenye mamlaka makubwa kwenye nchi hii.
“Tumekuelewa muheshimiwa”
“Asanteni
kwa kunielelewa, ila wapeni tahathari vijana wenu. Nitakuwa nikizunguka
zunguka kwenye kila mkoa na vituo vyote kisiri pasipo wao kujua, endapo
nitaumdua kuna ubadhilifu wowote kwa wananchi basi, kijana huyo au hao
watawajibika katika hilo. Asanteni kwa muda wenu”
***
“Mbona unatabasamu?”
Madam Mery alimuuliza mzee Godwin
“Kijana wangu, niliye potezana naye muda yupo hai”
“Ni nani?”
“John”
“John yupi?”
“Yule aliye kua mwanafunzi wako”
Furaha
ya mzee Godwin na Madam Mery ikazidi kuongezeka kwani mtu waliye kuwa
wanamtegemea kwenye mipango yao wamepata ujumbe wake kwa njia ya simu.
“Sasa yupo wapi?”
“Yeye mwenyewe hakuniambia kwamba yupo wapi ila atanijulisha kwamba yupo wapi”
“Sawa”
“Ila itabidi kuunda kikosi chenye nguvu na safari hii, Eddy nilazima afee”
Mzee Godwin alizungumza huku akiachia tabasamu pana usoni mwake, macho yake akiwa amemtazama Madam Mery.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment