NIGERIA: MWANADADA maarufu
kwenye tasnia ya muziki Barabi Afrika, Tiwa Savage amerudiana na
mumewe Teebillz baada ya kuachana naye kwa kile kilichodaiwa kuwa
mwanamme huyo anatumia madawa ya kulevya.
Imeelezwa kuwa, Teebillz amefanikiwa
kutibiwa kisiri katika kliniki ya tiba ya madhara yatokanayo na matumizi
ya madawa ya kulevya pamoja na kufanyiwa ushauri wa masuala ya ndoa
(Drug Addiction Rehabilitation & Series Of Marriage Counselling).
Kwa
mujibu wa televisheni moja ya nchini Nigeria humo iliyomfanyia
mahojiano Tiwa, imeeleza kuwa amerudiana na mumewe huyo kimya kimya bila
watu kujua kwa kile alichokieleza kuwa afya ya mumewe huyo inaendelea
kuimarika baada ya kutibiwa utumiaji wa madawa ya kulevya uliokuwa
umemuathiri kwa kiwango kikubwa, mbali na afya yake kuimarika, sababu
nyingine ni kwamba wawili hao wanataka wamlee kwa pamoja mtoto wao wa
kiume aitwae Ajmil.
Japo
bado wapo kwenye harakati za mwanzo kurudiana pole pole, huku uhusiano
wao ukionekana kuanza kuimarika upya siku hadi siku, wawili hao wamekuwa
wakionekana kwa pamoja wakienda kwenye kituo kimoja cha ushauri wa
masuala ya kisaikolojia na mambo ya ndoa jijini Lagos kwa ajili ya
kupata ushauri nasaha kuhusu ndoa yao.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment