MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Muheshimiwa tumemkosa”
Askari
walio agizwa kwenda kumfwatilia Mzee Godwin walikuja huku wakihema kana
kwamba ni kweli waliweza kumfwatilia ila ukweli ni kwamba walipo toka
ndani ya chumba cha walicho kuwepo na kwenda nje ya geti, wakatazama
kila upande na kushauriana wakimbie kimbie, kama nusu saa ili kuitoa
miili yao jasho, ili wakirudi watoe ripoti ya kwamba hawakufanikiwa
kumuona mzee Godwin. Eddy akawatazama kwa muda jinsi wanavyo hema
“Hamuna kazi, kuanzia sasa rudishni magwanda kwenye vituo vyenu vya kazi”
Askari hao wakabaki wamemtumbulia mimacho Eddy na mmoja akaanza kuangua kilio kikubwa cha kujutia
ENDELEA
“Muheshimiwa mimi kwetu ninategemewa, na mimi itetezi change ni hii kazi”
Askari
huyo alizungumza huku akiendelea kulia kwa machozi, Eddy hakuhitaji
kusikiliza kitu cha aina yoyote zaidi ya kuwasisitiza wakalilie mbele ya
safari kwani hawana sifa ya kuwa maaskari.
Hali
ya Phidaya ikaendelea kuwa tata huku daktari na manesi wakindelea
kuyastua mapigo ya moyo yaweze kufanya kazi, ila haikuwa rahisi kama
wanavyo zoea kufanya kwa wagonjwa wengine
“Dokta vipi?”
Nesi
Maria aliuliza huku akiwamgikwa na jasho jingi kwani nimara nyingi
wamejaribu kumstua Phidaya ila juhudi zao hazikuzaa matunda
“Atakuwa amekufa nini?”
Doktar
Khan alimuuliza nesi Maria kwa sauti ya chini ili waziri Eddy aliyopo
nje asiweze kusikia kinacho endelea ndani ya chumba hicho
“Hata mimi pia nahisi hivyo kwani si kawaida”
“Sasa utamuambiaje huyo waziri hapo nje?”
“Nani niwaziri?”
Nesi Maria alizungumza kwani kwa kipindi chote alicho kuwa anazungumza na Eddy hakujua kwamba ni waziri
“Mungu wangu, mimi sijajua……!!!”
“Ohooo hapo sasa na wewe unaharibu, mimi nimesikia watu hapo nje wakiangua vilio baada ya kuambiwa hawana kazi”
“Mmmmm ehee Mungu sijui itakuwaje”
Wakiwa
wakiendelea kujadilia, taratibu mashine ikaanza kuonyesha vimishale
viwili vya kijani ikiashiria mapigo ya moyo ya Phidaya ayamesha anza
kudunda japo kwa utaratibu bali anaashiria kwamba yu hai na si mfu kama
wanavyo hisi
“Ohhh asante Mungu wewe baba wa majeshi, hakuna lishindikanalo kwako”
Nesi Maria alisali kwani kupona kwa Phidaya ndio kupona kwa kazi zao wanazo zitegemea maishani mwao.
***
Upasuaji wa kutoa risasi zilizo kuwa kwenye kifua cha Madam Mery,
ukafanikiwa kwa kiasi kikubwa na madaktari wakafanikiwa kuweza kuzitoa
risasi hizo kwa usalama kisha wakamshona vizuri Madam Mery na kumpeleka
kwenye chumba maalumu cha wagonjwa mahututi. Kwa msaada wa mashine
akaendelea kupumua huku dripu la maji na damu yakiendelea kufanya kazi
ya kuongeza maji na damu vilivyo pungua mwilini mwa Madam Mery.
Usiku
wa manane Madam Mery akaweza kufumbua macho yake kwa mara ya pili,
kwani mara ya kwanza alikua wakiomba kuzungumza na Eddy, pale alipo pata
hofu kwamba anaweza kupotea maisha yake muda wowote kuanzia pale
Akayazungusha
macho yake kwenye kila kono ya chumba, kwaufahanu wake unao fanya kazi
vizuri akagundua kwamba pale ni hospitali. Pameni ya kitanda akaona kuna
kifaa maalumu ambacho ukikiminya nesi au daktari aliye karibu mtambo
huo wa kisasa unao weza kuwataarifu manesi na madaktari kwamba mgonjwa
wa chumba Fulani ana hitaji msaada.
Hazikupita dakika tano mlango wa chumbani kwakr ukafunguliwa na kuingia nesi mrefu kiasi aliye jazia maungo yake ya nyuma
“Nikusaidie nini?”
Nesi huyo alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Madam Mery.
“Eddy, Eddy waziri namuhitaji”
Madam
Mery alizungumza, kutokana na uwepo wa Eddy kwenye hospitali hii
uliwafanya watu wengi kuutambua uwepo wake. Hakuwa na kipingamizi nesi
huyo, aliye vaa kagauni kalisho ishia kenye maagoti na kuyafanay makalio
yake makubwa kutingishika vibaya mno kila anapo tembea
Nesi akaongoza hadi sehemu alipo Eddy, nje ya chumba, kwaheshima zote akasimama mbele ya Eddy
“Muheshimiwa kuna mwana mama anakuhitaji kwenye chumba cha wagonjwa mahuti”
Kabla
Eddy hajamjibu neno lolote nesi huyo mlango wa chumba alicho lazwa mke
wake, ukafunguliwa akatoka doktar Khan, akiwa na tabasamu usoni mwake
“Dokta vipi mke wangu?”
Doktar Khan akashusha pumzi nyingi kisha akaanza kuzungumza
“Tumejitahidi kadri ya uwezo na..”
“Mke wangu amekufa doktar?”
Eddy aliuliza kwa wasiwasi mwingi
“Hapana
hajafa, tumeweza kuyaokoa masha yake, ila kwa sasa atakuwa chini ya
uangalizi wa manesi watau, mutamuona kesho asubuhi kwa sasa nitaomba
mumuache apumzike”
“Sawa”
Eddy
alijubu kwa unyonge huku akitamni kuzungumza kitu kwa daktari huyo, ila
akajikuta akisahau ni kitu gani alihitaji kukizungumza. Hapakuwa na
jinsi yoyote ikambidi Eddy amuombe Mzee Mboho kukaa nje ya chumba hicho
hadi yeye pale atakapo rejea, yeye akaongozana nesi aliye kuja kumuita
na kufikishwa kwenye chumba alichopo Madam Mery
***
Mzee Godwin baada ya kutoka kwenye geti la hospitali akakodi taksi
iliyo mfikisha kwenye hoteli aliyo kuwa amefikizia na Madam Mery,
akaingia bafuni na kunyoo ndevu zake zote alizo kuwa nazo na kumfanya
arudi kwenye sura ya ukijana japo ni mzee, akakushanya nguo zake na
kuziingiza ndani ya begi alilo kuja nalo, akiamini anaweza kuifanya kazi
yake na kuimaliza ila hali tayari ilisha kuwa mbaya kwani mwanae Eddy
anamamlaka makubwa serikalini na endapo atamtia nguvuni nilazima
atahukumiwa.
Mzee
Godwin akatoa kwenye chumba cha hoteli na kuanza kutembea kwenye kordo
ndefu, hakuhitaji kutumi lifti kuhofia kukamatwa kizembe pale lifti
itakapo funguka na kukumbana na kundi la askari. Akaanza kushuka kwenye
ngazi akitokea gorofa ya saba kushuka chini, na kila mara akawa na kazi
ya kuchungulia chini kuona kama atakutana na mtu yoyote.
Mzee
Godwin akafanikiwa kufika nje ya hoteli pasipo kustukiwa akakodi taksi
nyingine na kumuomba dereva kumpeleka kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu
Julias K.Nyerere ili aweze kuondoka nchini Tanzania haraka iwezekanavyo
na kuelekea brazil alipo weka makazi yake ya maficho.
Mzee
Godwin akastushwa kukuta gari zipatazo sita za polisi zikiwa zimefunga
barabara ambayo walihitaji kupita kuelekea uwanja wa ndege. Na kundi
hilo la askari wote walionekana kuwa na silaha mikononi mwao na wawili
wakiwa namatochi makubwa yakiimulika taksi hiyo
***
Eddy akafungua mlango na kuingia ndani ya chumba alicho lazwa Madam
Mery na kumkuta akiwa yupo macho. Taratibu Eddy akaka kwenye kiti cha
pembeni ya kiti cha Madam Mery, huku akiwa na maswali mengi ni kwanini
amemkuta Madam Mery akiwa amepigwa risasi nyumbani kwake na kama alikuja
na mzee Godwin imekuwaje wameanza kushirikiana na mzee huyo. Ila
kutokana Madam Mery ni mngonjwa hakuhitaji kuuliza swali lolote zaidi ya
kusubiria kitu kilicho mfanya yeye kuitwa hapo
Madam
Mery alipo mtazama Eddy, akajikuta akimwagikwa na machozi, kila alivyo
lia maumivu kwa mbali akaanza kuyasikia kwani dawa ya maumivu aliyo
chomwa ndio ilikuwa ina kwenda kuishia kupoma.
“Eddy
kwanza nahitaji kukuambia kitu kitu kitakacho tokea muda wowote, Godwin
amepanga kutegesha bumu kwenye uwanja wa ndege wataifa na kuteka ndege
ambayo, atataka kuitumia kwa shuhuli zake binafsi”
Maneno
ya Madam Mery yakamfanya Eddy kustuka kwani hajafanikiwa kumtia
mikononi mzee Godwin, Eddy kwa haraka akaitoa simu yake mfukoni,
akajaribu kuiwasha akakuta imezima
“Mungu wangu”
Eddy
alionekana kuchanganyikiwa, akajaribu mara kadhaa kuiwasha simu yake
ila haikukubali kuwaka, kwa haraka akatoka nje ya chumba pasipo kumuaga
madama Mery kwa bahati nzuri akakutana na nesi aliye kuwa amemuita
“Lete lete simu yako”
Eddy alizungumza na kumfanya nesi huyo kuanza kujipapasa papasa ila akajikuta akishangaa
“Ahaa nimeicha kule mapokezi ninaichaji”
Alizungumza
na kuanza kukimbi kuelekea mapokezi, huku Eddy akifwata kwa nyuma. Kila
walio pishana naye alihisi kuna jambo linalo endelea, wakafika kwenye
chumba cha mapokezi, nesi huyo akaingia ndani naichomo simu yake kwenye
chaji na kumkabidhi Eddy aliye onekean kuchanganyikiwa.
“Unafunguaje hiii”
Eddy
alizungumza baada ya kushindwa kufungua mfuniko wa simu ili kuweza
kubadilisha line za simu na aweke yakwake. Nesi akamsaidia kufungu simu
hiyo, kisha akatoa line yake na kumpa Eddy, akaweka line yake na kuchua
batrii na kuiweka na kuiwasha simu hiyo pasipo pasipo kuurudishia
mfuniko wa nyuma. Eddy kwa haraka akatafuta namba ya mkuu wa polisi,
kisha akaipiga. Ikaita kwa muda na kupokelewa na sauti iliyo jaa
usingizi
“Haloo”
“Kuna tukio la ugaidi lanataka kutendeka muda wowote kuanzia sasa, huku uwanja wa ndege wa JK unatakla kulipuliwa”
Eddy alizungumza kwa haraka haraka huku akihema
“Wewe nani kwani?”
Mkuu wa askari aliuliza
“Unataka kunijua mimi ni nani?”
“Ndio kwa maana wewe ugaidi Tanzania utokee wapi, hembu acha upuuzi wako. Acha tulale sisi”
“Kabla hujakata simu, kuanzia sasa huna kazi pumbavu wewe. Unazungumza na waziri wa Ulinzi Eddy, Eddy Godwin”
“Muhe……”
Eddy
akaakata simu na kutafuta simu ya makamu msaidizi wa kamanda huyo wa
kanda maalumu, akaipiga namba hiyo hata sekunde tano hazikupita, simu
ikaokelewa
“Ndio muheshimiwa”
Kamanda huyo alizungumza kwa wasiwasi mwingi, na kumuomba dereva wa gari anaye muendesha kusimamisha pembeni
“Kuna
tiukio la uwanja wa ndege kulipuliwa hakikisheni munafunga barabara ya
kwenda uwanja wa taifa na gari zote munazisimamisha na kuzikagua na
mumkamate Godwin aliye kuwa mkuu wa jeshi la ulinzi”
“Sawa mkuu nimekuelewa, kwanza nipo doria muda huu na vijana”
“Fanya hivyo kuanzia sasa hivi unachukua nafasi ya mkuu wako, nimefukuza kazi muda huu”
“Ohh asante sana muheshimiwa”
Eddy
akakata simu, akakata simu na kumpigia simu mkuu wa ulizi katika uwanja
wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere, simu yake nayo ikapokelewa ndani ya
muda mchache
“Haloo”
“Panga vijana wako, waimarishe ulizi kunahatihati ya uwanja wa ndege kulipuliwa kwa bomu”
“Haaaa…..!!!”
“Unashangaa nini?”
“Hapana nimekuelewa muheshimiwa”
Kilicho
muokoa mkuu huyu kuto fukuzwa kazi ni kuweza kuikumbuka sauti ya Eddy
aliyo toka kuisikia kwenye bunge mida ya saubuhi na wala hakufahamu
namba yeka waziri huyo ameitolea wapi. Hakutaka makuu zaidi ya kupiga
simu kwenye sekta nzima za ulinzi uwanja wa ndege kuwaamuru askari
kudumisha ulinzi kwa anaye ingia na kutoka na kila waliye mtilia mashaka
akamatwe kwa mahojiano
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment