“Kwanini Diamond anapendwa? Diamond hapendwi si sababu ya kubeba vyuma
tu, unaweza ukabeba vyuma na usipendwe vilevile. Angalia muziki wa
Diamond kwanini unapendwa. Diamond anapendwa si kwaajili ya skendo
kwasababu zile skendo pia huwa zinamuumizaga. Jamaa anatengeneza muziki
mzuri, kubali ukatae,” alisema Bella kwenye mahojiano na Lake FM ya
Mwanza.
“Mimi napenda anayefanya vizuri. Mimi kila nikitaka kutoa ngoma lazima napima ngoma ya Diamond, nitaangalia anaimba nini, kwanini watu wanampenda? Naangalia Alikiba, kwanini watu wanampenda, kaimba nini, naanza kupima ngoma zao. Halafu mimi natafuta, sio niimbe kama Diamond, sio nifanye kama Alikiba, natafuta njia pale katikati. Ukitaka baraka wakubali kwanza wanaokubalika,” alisisitiza Christian Bella

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment