Katika
nafasi yake ya Mjumbe Maalum wa Kamisheni hiyo, Rais Mstaafu
amemkabidhi Waziri Mkuu wa Ethiopia Ripoti ya Kamisheni hiyo yenye
mapendekezo ya namna Dunia inavyoweza kukabili janga la Elimu kwa
kuwekeza katika Mpango wa Kizazi cha Elimu (A Learning Generation).
Mpango
huo unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya Elimu katika nchi
zinazoendelea ndani ya Kizazi Kimoja (miaka 30). Azma kuu ya Mpongo huo
ni kuwezesha ifikapo mwaka 2040, watoto wote kote duniani wawe wanaopata
elimu iliyo bora na kwa kiwango kinachofanana dunia nzima.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo, kwa sasa, hali ya elimu katika nchi
zinazoendelea inalingana na ile ambayo nchi zinazoendelea zilikuwapo
miaka 70 iliyopita. Aidha, ripoti inasisitiza kuwa, ikiwa nchi
zinazoendelea zitaendelea kwa kasi ya sasa, itazichukua nchi hizo kati
ya miaka 90 na 110 kufikia viwango vya sasa vya nchi zilizoendelea.
Kwa
ajili hiyo, Kamisheni inapendekeza njia mpya na bora za kufanya mageuzi
katika elimu ikiwemo kuongeza usimamizi, kupanua fursa, kuingiza
ubinifu na teknolojia na kuongeza uwekezaji katika elimu kwa kushawishi
ushiriki wa Jumuiya ya Kimataifa na Sekta Binafsi. Iwapo mapendekezo
hayo yatatekelezwa, nchi zinazoendelea zinaweza kufikida pengo hilo
ndani ya miaka 30 ijayo.
Rais
Mstaafu ameiomba Ethiopia kujiunga na Mpango huo ambapo Waziri Mkuu wa
Ethiopia ameelezea nia ya nchi yake kujiunga na Mpango huo.
Ethiopia
ni moja kati ya nchi za Afrika ambayo imepiga hatua kubwa katika utoaji
wa fursa ya elimu kwa watoto na vijana wake. Pamoja na mafanikio
makubwa bado zipo changamoto zinazohitaji hatua madhubuti ili kufikia
lengo la kizazi cha elimu ifikapo 2040.
Ziara
ya Rais Mstaafu itamfikisha katika nchi 14 barani Afrika ambapo
zimechaguliwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo. Tayari
amekwishazitembelea nchi za Uganda na Malawi na kufanya mazungumzo na
viongozi wakuu wa nchi hizo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment