Loading...

MAITI Sita Zakutwa Zikielea Kwenye Mto Ruvu Bagamoyo Huku Zikiwa Zimeoza Vibaya

Maiti sita ambazo hazijatambulika zimekutwa zikielea katika Mto Ruvu eneo la Bagamoyo, Mkoa wa Pwani zikiwa zimehifadhiwa kwenye mifuko ya Sandarusi maarufu viroba vya uzito wa Kilogramu 200, huku zikiwa zimeharibika vibaya.

Diwani wa Kata ya Makurunge, Paul Kabile alisema maiti hizo ambazo ni za jinsia ya kiume ziligunduliwa na wavuvi

Kabile alisema maiti tano ziligunduliwa Desemba 6 majira ya alfajiri kwenye Kitongoji cha Kitopeni wilayani Bagamoyo, ambako wavuvi hao waligundua miili hiyo wakati wakiendelea na shughuli zao kwenye Mto huo

“Maiti hizo kila moja ilikuwa imehifadhiwa kwenye kiroba huku zikiwa zimewekewa mawe na mifuko hiyo ikiwa imeshonwa juu kama vile yamehifadhiwa mahindi au mchele”.alieleza

Kabile alisema kuwa wavuvi hao baada ya kuziona maiti hizo walizizika kutokana na kuharibika sana na kushindwa kuzipeleka hospitali kuzihifadhi.

“Wavuvi hao walizizika maiti hizo huku kukiwa hakuna taarifa yoyote juu ya kuwa zimetoka wapi na ni watu gani waliofanya tukio hilo”, alisema Kabile na kubainisha kuwa maiti nyingine moja iligunduliwa jana.

Mwandishi wa habari wa jeshi la polisi Mkoa wa Pwani, Hassan Mtengevu, alithibitisha kutokea tukio hilo, na kueleza kuwa wanafanya uchunguzi kwa kushirikiana na daktari ili kufahamu watu hao walikufa kwenye mazingira gani.

Source: Habari Leo

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright KISWAGA BLOG
Back To Top