Young Dee amesema hafikirii kwa sasa kufanya jitihada za kwenda international wakati nyumbani bado hajapenya ipasavyo.
Dee anasema anachoamini ni kuwa msanii hawezi kufanya vizuri kimataifa kama nyumbani bado hafanyi vizuri.
“Kuna sehemu mimi sijafika bado Bongo nahisi, Tanzania ni nchi kubwa sana, kuna East Africa halafu kuna Africa halafu ndio kuna kimataifa. Lazima uanze huko,” Young Dee alimuambia mtangazaji wa Lake FM ya Mwanza, Haroun Tambwe.
“Kabla sijafikiria kujulikana kimataifa, lazima nianze kwanza East Africa ili Tanzania nihakikishe nimetoboa. Kule watakuwa na sababu ya hata kuniassociate na muziki wao kwasababu nitakuwa nakubalika nyumbani
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment