Loading...

YALIYOMPATA Kala Jeremiah Mwaka 2016 Huaya hapa



Msanii wa Hip Hop na mwana harakati kutoka jijini Mwanza Kala Jeremiah amesema 2016 ni mwaka mkubwa sana kwenye maisha yake kutokana na mafanikio alio yapata.

Akitoa salamu za mwaka mpya kwa mashabiki wake kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Kala amesema "kwanza nilipata mtoto, ambacho ni kitu kikubwa sana maishani mwangu maana ndiyo mtoto wangu wa kwanza. Baada ya kupata mtoto nili udedicate huu mwaka kwa watoto kwa ujumla na kwa asilimia 99 nimefanya sana kazi zinazowahusu watoto kwa ujumla na malengo yangu yametimia kwa kweli. Niliamua kuweka nguvu zangu kubwa kwa watoto na nimepata mafanikio makubwa sana katika kutekeleza nilio yatekeleza".

Kala ambaye ameutumia nusu ya mwaka 2016 akiwa anafanya kazi za watoto amesema ni kitu kikubwa alichokifanya kwenye maisha yake ikiwemo kutoa wimbo wake wa 'Wana ndoto' aliomshirikisha Miriam uliokuwa na lengo la kubadili maisha ya watoto wanaoishi kwenye maisha duni na magumu na ambao wanapitia vikwazo mbalimbali huenda ni kwa kukosa Wazazi, walezi au kutengwa na jamii

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright KISWAGA BLOG
Back To Top