Loading...

SORRY MADAM -Sehemu ya 11 & 12 (Destination of my enemies)


 MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“Mama mbona siwaelewi”
“Huo ndio ukweli halisi mwanangu, wewe si mtoto wa Godfrey, baba yako wewe ni Godwin. Am your mother na natambua ni nani aliyenipa ujauzito wako”
Eddy akajikuta akishusha pumzi huku macho yakiwa yamemtoka kiasi kwamba akawa anajihisi kuchanganyikiwa kwani si jambo rahisi kwani anavyo tambua kwamba baba yake halisi ni Godfrey
“Unataka kujua ukweli eheee?”
Mama Eddy alizungumza kwa uchungu mkubwa huku wakitazama na mwanye, hadi baadhi ya wauguzi wakaanza kuyatega masikio yao kuweza kusikia ni kitu gani mama huyo anahitaji kukizungumza kwa mwanaye huyo

ENDELEA
“Mama”
Eddy alimuita mama yake kwa sauti ya chini, akaupitisha mkono wake mmoja kwenye bega la mama yake na kumkumbatia huku akiendelea kusononeka

“Eddy natambua kwamba Godfrey alikuambia mambo mengi kuhusiana na sisi, ila yote aliyo zungumza kwako ni uongo mwanangu”
Mama Eddy aliendelea kuzungumza huku  machozi yakiendelea kumwagika, macho ya Eddy yakazunguka kwenye eneo walilopo na kuwastua wauguzi wa kike ambao mara kwa mara waliweza kuwatazama. Eddy akamnyanyua mama yake na kuongozana naye hadi lilipo gari lake na kuingia ndani. Akafunga vioo vyote vya gari ili sauti isitoke nje

“Mama nimesha kua sasa, nahitaji kujua ukweli wa kila kitu kuhusiana na yupi ni baba yangu kati ya Godwin na Godfrey?”
Mama Eddy akashusha pumzi nyingi, huku taratibu akiipa nafasi akili yake kuweza kuvuta kumbukumbu zake za nyuma.

        ******
 Miaka arobaini na tano iliyo pita, nilikuwa ni binti mzuri sana mwenye kuvutia machoni mwa wengi, nilikuwa ninapendezeshwa na mama yangu, kila asubuhi nilipo kuwa ninaamka.

Kipindi hicho nilikuwa ninami mitatu, jambo ambalo liliwafanya wazazi wangu kwa kipindi kile kuweza kunianzisha masomo ya chekechea. Ilikuwa ni furaha kubwa kwangu mimi, kuweza kuanza shule mapema kiasi hichi, ila nilijikuta ninakuwa kivutio kwa wanafunzi wengine wakiwemo Godwin na Godfrey, ambao nao pia walikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa chekechea niliyo kuwa ninasoma, Godwin na Godfery walitokea kuwa marafiki zangu sana, hii nikutokana na kufanana kwao. Kila mmoja alikuwa na sifa zake za kipekee

Godwin yeye alikuwa ni mcheshi, mpenda michezo, mteteaji. Alikuwa ananitetea kila pale nilipokuwa ninaonelewa na baadhi ya wanafunzi wezetu ambao walikuwa wakizivuta nywele zangu nilizokuwa nimesukwa mabutu mabutu.

Ila Godfrey alikuwa ni mvivu darasani, alikuwa hapendi michezo na mara nyingi alikuwa anapenda kukaa na wasichana wengine, jambo lililo kuwa likitukera mimi na Godwin. Tulibahatika kusoma shule ya msingi pamoja, hadi tunafika sekondari sote tukawa katika shule mmoja. Ila Godfrey alikuwa bize na visichana wengine. Nilimpenda sana Godfrey nikawa ninawivu naye japo sikumueleza ukweli kwamba ninampenda sana na kumuhitaji. Godwin alinipenda sana kiasi kwamba sikuwa na jinsi zaidi ya kujikuta nikimpenda Godwin.

Tulipo maliza kidato cha nne mimi nilibahatika kwenda kusoma Uingereza, kutokana baba yangu alikuwa na uwezo na pia alikuwa ni mwanasheria mkuu wa kipindi hicho. Nilikaa Uingereza kwa miaka nane. Kwakipindi chote sikuwa na mawasiliano kati ya Godwin na Godfrey, ila nilikuja kusikia kwamba baba yao alifariki kwa ugonjwa wa sartani ya damu. Na sikuweza kujua ni wapi walipo. Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuwatafuta ila sikuweza kupata mafanikio.

Nilipo anza kazi ya udaktari kwenye kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Muhimbili, ndipo kuna siku kulitokea ajali ya basi, hapo ndipo nilipo weza kumpata Godwin, akiwa ni miongoni mwa majeruhi wa ajali hiyo.

Godwin alikuwa mahututi, ilinilazimu kumfanyia upasuji mimi na madaktari wezangu, Alipo pata nafuu, mapenzi yetu yakafufuka upya. Ndipo nilipo amua kuanza kuishi naye nikiwa katika mapenzi mazito, ndipo alipo mleta Godfrey kuja kuishi nasi pale nyumbani. Godwin kwa kipindi hicho alikuwa nimwanajeshi, na alikuwa anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo mbalimbali. Ninakumbuka alipangiwa safari ya kwenda Pakistani, huko walipangiwa kwenda kukaa kwa kipindi kisicho julikana.

Ulikuwa ni usiku wa fauraha na majonzi mimi na Godwin, pale tulipo kuwa kitandani, kwani ilikuwa ni muda mchache tangu tufunge ndoa yetu. Siku hiyo ndio siku ambayo nilikuwa kwenye  siku za hatari kama mwanamke, aliye kamilika, niliweza kuzipokea mbegu za Godwin, na kujua kabisa zimekwenda kuingia kwenye mfuko wangu wa uzazi. Asubuhi ya siku iliyo fwata tulimsindikiza Godwin hadi kwenye uwanja wa ndege
“Gody, mlinde shemeji yako, najua ninapo kwenda nipagumu sana, ila ningependa nirudi nimkute mke wangu akiwa salama”

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright KISWAGA BLOG
Back To Top