Darassa
Alianza kuvuma zaidi kuanzia Januari
alipoibuka na Wimbo wa Kama Utanipenda kisha akatoa Heya Haye na Too
Much. Kwa sasa Wimbo wa Muziki umemfanya azidi kung’ara.
Mwaka huu, amevuma tena hasa alipotoa
Wimbo wa Aje. Ameshiriki tuzo nyingi zikiwemo, HiPipo (Uganda), AFRIMA
(Nigeria), MTV EMA (Uholanzi) pamoja na EATV (Tanzania).
Alianza kuvuma kuanzia Juni alipoibuka
na Wimbo wa Hainaga Ushemeji uliokuwa na mahadhi ya Singeli. Kuibuka
kwake kukaupa hai muziki huo na kuwafanya vijana wengi nao kuibuka.
Wimbo wa Ndi Ndi Ndi uliotoka Machi
mwaka huu umemfanya kuvuma na kumpa shoo nyingi kupitia ziara yake ya
Naamka Tena. Bado anaendelea kuvuma na Wimbo wa Sawa na Wao.
Bella
Tangu atoa nyimbo zake zikiwemo
Nagharamia, Nani Kama Mama. Bella bado anaendelea kuvuma hadi sasa.
Licha ya kuachia Wimbo wa Nishike, amekuwa miongoni mwa wasanii
wanaoendelea kupiga shoo za pesa ndefu.
Navy Kenzo
Wawili hawa wanaounda kundi hili, Aika
na Nahreel wameendelea kuvuma hasa mwezi Juni walipotoa Wimbo wa
Kamatia. Wamelamba mikataba kibao.
Raymond
Ni zao kutoka Lebo ya Wasafi Classic
Baby (WCB). Amevuma kupitia Wimbo wa Kwetu na Natafuta Kiki na Salome
alioshirikiana na Diamond.
FA
Alivuma kuanzia mwezi Juni alipofunga
ndoa na mzazi mwenzake anayefahamika kwa jina la Helga. Kwa sasa
anaendelea kuvuma zaidi kupitia Wimbo wa Dume Suruali.
Vanessa
Amezidi kujihakikishia kuwa ni miongoni
mwa mastaa wa kike wa Muziki wa Bongo Fleva wanaoutambulisha kimataifa.
Kwa mwaka huu ameshiriki tuzo nyingi za kitaifa na kimataifa zikiwemo
HiPipo (Uganda), Soundcity (Nigeria), NEA (Nigeria), MTV Africa (MAMA),
(Afrika Kusini) na EATV (Tanzania).
Diamond
Ameendelea kuvuma tena mwaka huu. Licha
ya kumsainisha msanii Rich Mavoko katika lebo yake ya WCB ameendelea
kutikisa kwenye nyimbo zake ikiwemo Kidogo akiwa na P-Square, Salome
akiwa na Raymond. Ameshiriki katika tuzo nyingi za kitaifa pamoja na
kupataza ziara na wasanii wakubwa nchini Marekani akiwemo, Ne-Yo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment