ZIMBABWE: Chama tawala ZANU-PF kimemtangaza Rais Robert Mugabe(92) kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2018
Mugabe mwenye umri wa miaka 92 sasa amekuwa kiongozi wa taifa hilo tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980 kutoka kwa Wakoloni Waingereza.
Mbali na ZANU-PF kumemtangaza Rais
Robert Mugabe kuwania tena kiti hicho, kuna baadhi ya makundi yameibuka
huku yakipinga mkongwe huyo kuendelea kuliongoza taifa hilo kwa madai
kuwa ameshusha uchumi wa nchi.
Mugabe anasifika kwa kuwa rais mwenye
misimamo thabiti licha ya kuwa mzee, lakini akisimamia jambo na kuamua
lifanyike lazima lifanyike na hata kama akikataa jambo anamaanisha
amekataa haswa. Hateteleki, hamuogopi mtu wala taifa lolote.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment