Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Asha Saidi, hivi karibuni alikiona cha moto baada ya kufumwa akiiba mashuka na deki kwenye nyumba ya jirani yake.Tukio hilo lilitokea mtaa wa Mawenzi ambao mama huyu anaishi, inadawa aliruka ukuta na kukutwa na mama mwenye nyumba anayeitwa Zainabu akifanya uhalifu huo.
Ilidaiwa kuwa baada ya Zainabu kushuhudia tukio hili alipiga kelele za mwizi ndipo watu walipojitokeza na kumtaiti.Hata hivyo, wakati mwanamke huyo akiwa chini ya ulinzi wa raia, polisi walifika na kumtia nguvuni na alipoulizwa sababu ya kuiba alijitetea.
“Jamani naomba mnisamehe ninaumwa na maisha yangu ni magumu, nasumbuliwa na Malaria hivyo niliona njia ya kujipatia matibabu ni hii kwani sikuwa na hela kabisa,” alisema Asha.
...Akiwa mikononi mwa polisi.
Wapangaji waliokuwa kwenye nyumba hiyo walisema kuwa kabla ya tukio
hilo jana yake kulitokea wizi wa simu ambayo ilisababisha mtafaruku
baina ya wapangaji lakini hawakumpata mwizi hivyo wakadai huenda Asha
alihusika.Hata hivyo, polisi waliofika eneo la tukio walimchukua
mwanamke huyo na kumpelekea kituoni kwa mahojiano zaidi.Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment