Leo ni mara ya pili kwa wafuasi na wanachama wa chama hicho kutwangana makonde mahakamani wanapofika kusikiliza kesi inayozihusisha pande mbili za chama hicho.
Pande hizo ni kati ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.
Ugomvi huo ambao umewahusisha walinzi wa viongozi wa chama hicho maarufu kama mabaunsa wa pande hizo mbili umezimwa na askari polisi sasa hivi.
Kwa sasa wafuasi wa pande zote wameingia mahakamani wanasubiri jaji aingie kwa ajili ya kusoma ya kusoma uamuzi wa maombi ya upande wa Maalim Seif kumtaka Jaji Sekieti Kihiyo anayesikiliza kesi hiyo ajiondoe kwa madai kuwa hawana imani naye.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment