Loading...

Tumbuatumbua ya Magufuli yailiza tena familia ya Malecela!

magufuliRais John Magufuli
  • Matamko yawaponza Anne na Mwele
Na Walusanga Ndaki/GPL
DHAMIRA ya Rais John Magufuli kutaka kuwarudisha Watanzania katika msitari wa utendaji wa kiadilifu – bila kujali majina, vyeo au hadhi yoyote katika jamii – imepeleka kilio kingine tena kwa familia ya kiongozi mstaafu John Samwel Chigwiyemisi Malecela.
Safari hii, kilio kimeingia katika nyumba ya Mzee Malecela kupitia kwa binti yake Mwele Malecela ambaye aling’olewa katika nafasi hiyo juzi na Rais Magufuli kutokana na mkanganyiko aliousababisha kuhusiana na ugonjwa wa Zika.
Mwele alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ambapo kilichomwangusha ni kutangaza moja kwa moja matokeo ya utafiti wa ugonjwa wa Zika nchini, jambo ambalo linatakiwa kufanywa na Wizara husika ya Afya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya kimataifa.
mwele                                                                                          Mwele Malecela
Kutenguliwa kwa mkurugenzi huyo ambaye nafasi yake imeshikwa na Profesa Yunus D. Mgaya, kulitokana na tamko lake juu ya kuwepo kwa ugonjwa huo nchini ambalo lilichapishwa katika vyombo mbalimbali vya habari, na kuzua tafrani miongoni mwa jamii kuhusiana na ugonjwa huo hatari unaoitishia dunia.
Tamko la mkurugenzi huyo wa NIMR limepingana na mamlaka zote zingine zinazohusiana na masuala ya afya ambapo Mganga Mkuu  wa Serikali, Profesa Bakari Kambi, alikanusha kuwepo kwa ugonjwa huo nchini ambao katika tamko la NIMR lilisema tayari umeonekana katika mikoa ya Kanda ya Ziwa huko Geita, Kagera na Mara.
Kwa mujibu wa mamlaka za afya, taarifa za ugonjwa wowote hatari  duniani ni lazima zitolewe kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Tukirudi nyumba, simanzi kuu ya kwanza iliyoikiumba familia ya Malecela kisiasa tangu kuanza kwa utawala wa Magufuli ni pale ambapo mke wa mkongwe huyo wa siasa nchini, Anne Kilango Malecela, alipong’olewa katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga siku chache tu baada ya kuapishwa.
anne                                                                                                                 Anne Kilango Malecela
Kilichomng’oa mama huyo katika nafasi yake ni suala la wafanyakazi hewa ambapo tamko alilotoa kwamba mkoa wake haukuwa tena na wafanyakazi hewa – wakati walikuwa bado wapo – lilimgharimu nafasi hiyo na “kumrudisha nyumbani”.
Kinachoonekana wazi ni kwamba kina mama hao wawili wa familia ya Malecela, wameponzwa na kitu kinachofanana — matamko yao!  Kutumbuliwa kwao kunatokana na kufanya matamko ya haraka yasiyokwenda sambamba na hali halisi, hivyo kuwagharimu kazi zao.
Mzee Malecela ambaye ni mmoja wa wakongwe wa kisiasa wachache waliobaki na ambao walishiriki harakati za kupigania uhuru wa nchi hii bega kwa bega na hayati Mwalimu Nyerere, aliwahi kushika nyadhifa nyingi za kisiasa nchini zikiwemo, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Uchukuzi, Balozi Uingereza, na kadhalika.
malecela                                                                                                                  Mzee John Malecela
ZIKA NI NINI?
Ugonjwa wa Zika ni ugonjwa unaoenezwa na mbu aina ya Aedes ambao husababisha homa kali kwa wagonjwa na matokeo yake kwa kina mama wajawazito ni kuzaa watoto wenye vichwa vidogo.  Wataalam wanasema ugonjwa huo ulianzia katika mizitu ya Zika nchini Uganda,  na ndiyo maana ukapewa jina hilo.  Ugonjwa huo ambao ulikuwa haufahamiki kwa watu wengi unasemekana ulienea sehemu mbalimbali duniani kutokana na safari za watu.
Utafiti wa kitaalam zaidi uliofanywa duniani, uligunduliwa na kufahamika vyema mara ya kwanza Brazil ambapo ya athari zake kuu zilizoanza kufahamika mapema ni watoto kuzaliwa na vichwa vidogo.
MJUE MWELE MALECELA
Mwele Ntuli Malecela aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) alizaliwa Machi 26, 1963 jijini Dar es Salaam.
Elimu yake ilimfikisha hadi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikosomea masuala ya wanyama (zoology) na baadaye kujiunga na MIRI mwaka 1987 ambapo kiuto cha kazi yake kilikuwa Amani, Tanga, alikoendesha utafiti wa magonjwa ya binadamu.
Baadaye aliendelea na elimu yake kwenye chuo cha  London School of Hygiene & Tropical Diseases na kupata shahada ya MSC mwaka 1990 na shahada ya PhD mwaka 1995.  Aliendelea na utafiti akiwa NIMR na akawa Mkurugenzi wa Utariti, Uratibu na Uendelezaji (DRCP) mwaka 1998 na kisha kuwa Mkurugenzi wa Mpango wa Magonjwa ya Binadamu (Lymphatic Filariasis) mwaka 2000, mpango ambao hivi sasa unafanya kazi katika wilaya 53 (ukujumuisha watu milioni 13).
Aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR mwaka 2010 akiwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hii.  Mnamo Juni 2015, alichukua likizo maalum kwa ajili ya masuala ya kisiasa akiwa amejiunga na Chama Cha Mapinduzi mwaka 1981.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright KISWAGA BLOG
Back To Top