Mwanamitindo ambaye
hivi karibuni amekuwa gumzo kutokana na umbo lake, Jane Rimoy ‘Sanchi’
amefungukia mambo mawili ambayo kila akiyakumbuka hujikuta akibubujikwa
na machozi.
Akizungumza na Ijumaa hivi
karibuni juu ya maisha yake kwa sasa, Sanchi ambaye awali alikuwa
akifahamika kwa jina la Sanchoka alisema kuwa, anajisikia furaha
kutokana na jamii inavyomjadili na kusema kwamba, huenda amepewa umbo
alilonalo kwa makusudi.
“Nina
furaha na maisha yangu, najua kuna baadhi wanakwazika na life style
yangu lakini mimi niko poa,” alisema Sanchi na kuongeza:
“Ila kuna wakati huwa nalia
ninapokumbuka baadhi ya matukio ambayo yaliniumiza sana. Kwanza
nakumbuka nikiwa na umri wa miaka sita, nilinusurika kubakwa na rafiki
wa mjomba wangu. Nisingependa kulizungumzia sana hili kwa kweli.
“Pia huwa nalia sana nikimkumbuka
marehemu baba yangu. Miaka 14 imepita tangu baba yangu afariki lakini
bado siamini kama siko naye. Alikuwa akinipenda sana lakini Mungu
akampenda zaidi,” alisema Sanchi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment