OFISI YA MBUNGE Jimbo La Mikumi inalaani sana kitendo cha kinyama
kilichofanywa na Ndugu zetu wa jamii ya wafugaji kwa kujichukulia sheria
mkononi na kumjeruhi vibaya Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji
cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi
ambapo leo tarehe 25 Desemba majira ya Mchana amechomwa mkuki mdomoni
na kutokezea nyuma ya shingo yake, ambapo alipelekwa hospitali ya
wilayani Kilosa na baadae amekimbizwa hospitali ya mkoa Morogoro ili
kufanyiwa operesheni ya kuondoa mkuki huo na kwa matibabu zaidi.
Augustino Mtitu alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa
akimsaidia jirani yake kufukuza Ng'ombe wasiharibu mazao shambani kwake,
Kipande cha mti kinachoonekana hapo mdomoni ndiyo mkuki uliokatwa ili
kupunguza urefu wa mkuki huo wakati wakimkimbiza hospitali, Inasemekana
MwenyeKiti wa kijiji na MwenyeKiti wa kitongoji hicho nao wamejeruhiwa.
WITO KWA SERIKALI.
Ofisi Ya Mbunge Mikumi inatoa wito kwa Serikali kuwabaini wale wote
waliofanya kitendo hiki cha kinyama kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali
za kisheria ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia sheria
mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu mkubwa wa Amani na migogoro
isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA.
Imetolewa na:-
Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Mikumi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
Post a Comment