Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana
tarehe 24 Desemba, 2016 amewasili mkoani Singida na kupokelewa na mkuu
wa Mkoa wa huo Dkt. Rehema Nchimbi na viongozi mbalimbali wa mkoa wa
Singida.
Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, leo tarehe 25 Desemba 2016 wanatarajia kuungana na waumini wengine wa dini ya Kikristo nchini katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi mkoani Singida.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaomba
waumini wa dini ya kikristo mkoani Singida kujitokeza kwa wingi
kuungana na Rais Magufuli katika ibada ya Krismasi kwani imekuwa ni
heshima kwao kutokana na uwepo wa Rais Mkoani hapa kwa ajili ya sikukuu
ya Krimass.
Dkt.
Nchimbi amewataka wananchi wa mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla
kuendelea kumuombea Rais Magufuli na familia yake ili aendelee
kuwatumikia watanzania katika kuwaletea maendeleo.
Amesema
ni bahati kubwa kwa mkoa wa Singida kwa mara nyingine tena kumpokea
Kiongozi huyo Mkuu wa nchi kwa kuwa katika kipindi kifupi mkoa huo pia
ulimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Kassim Majaliwa alipohudhuria sherehe za Maulidi.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Singida
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini
Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Singida na kupokelewa na
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akielezea ujio wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mkoani humo
ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki katika Ibada ya Siku ya
Krismasi katika Kanisa mojawapo mkoani Singida.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment