MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
Televishen
pamoja na Tv zote nchini Tanzania, zipo hewani, kuweza kuyanyakua
mazungumzo ya moja kwa moja ya Raisi Praygod Makuya, kwenye uteuzi wa
mawaziri wapya, hii ni kutokana na waziri mkuu kuweza kujiudhulu, kwa
kusumbuliwa na matatizo ya kiafya yaliyo mchukua kipindi kirefu kukaa
nje ya ofisi pasipo uwepo wake. Kama kanuni na taratibu za nchi ya
Tanzania, inamlazimu raisi kuweza kufanya hivyo punde tu waziri mkuu
anapokuwa ameachia kiti hicho kinacho tamaniwa na kila kiongozi aliyopo
serikalini.
Raisi
akaanza kutaja majina ya mawaziri wapya watakao chukua nafasi za
mawaziri walio punguzwa kwenye wizara mbalimbali. Masikio ya wananchi
wengi wa Tanzania, ni kwenye wizara ya ulinzi, ambayo katika siku za
hivi karibuni imetokea kuyumba, hadi wananchi kuanza kupoteza imani na
serikali yao pamoja na jeshi zima la polisi. Majina kadhalika ya
mawaziri wapya na wazamani walio badilishwa wizara ya kaendelea kutajwa,
ikafikia kwenye wizara ya ulinzi ulinzi, hapa raisi akanyamaza kidogo
na kumeza fumba la mate huku akizikodolea kamera zilizopo mita chache
kutoka katika sehemu aliyo simama.
“Katika
wizara ya ulinzi, nimeweza kufanya mabadiliko makubwa sana, ambayo
ninaamini yatakwenda kufurahiwa na wananchi walio wengi. Kwa maana
katika kipindi changu cha utawala nimeweza kupokea malalamiko mengi sana
kuhusiana na uhalifu katika jamii inayo tuzunguka.”
“Wizara hii nimeweza kuweka watu hodari, wanao weza kuhakikisha wanafuta hofu yote iliyo jengeka katika mioyo mingi ya wananchi”
“Basi hapa waziri wa wizara hii, anaitwa Eddy Godwin, makamu wake atakuwa Bernad Ngoswe”
Wananchi
wengi wakabaki wakiwa wameshangazwa na jina hilo kwani, hawajawahi
kulisikia kwenye serikali tangu raisi Praygod kuingia madarakani.
“Hivi huyo Eddy Godwin ni nani?”
Mchaga
mmoja alisikika akiwauliza wezake walio kusanyika katika duka lake la
kuuza tv, redio na vitu vingine vya majumbani, lililopo maeneo ya
Kariakoo.
“Hata mimi simfahamu”
“Hawa watakuwa wanagawiana, kwanini wasimpe yule….yule nani….”
“Chande?”
“Hapana yule, ambaye wamekwenda kumtupia kwenye kilimo”
“Ahaaaa Masele”
“Ehee huyo huyo, yule jamaa anaonekana yupo fiti sana”
“Yaani wee acha. Ila baadaye si wanaapishwa, tutakuja kumcheki huyo jamaa mwenyewe”
“Etieee”
“Naye asije akatuletea ufala kama huyu mwenzie aliye pita Haki ya Mungu, naye tutamuombea mabaya”
“Hahaaa maswawe punguza munkari bwana”
“Sio
munkarti chalii yangu, yaani waziri akiwa ovyo hata hawa watendaji wake
huku chini wote wanakuwa mambumbu, hembu nenda pale sentral kaseme
unatatizo uone kama hawata taka rushwa”
Nazungumzo
ya watu mbalimbali katika mitaa tofauti ndani na nje ya jiji la Dar es
Salaam, yalikuwa ni kuhusiana na huyo waziri mpya waliye msikia jina
lake likitajwa. Wengi wao hawakuonyesha imani yoyote kwa waziri huyo,
wanaamini naye atafanya madudu kama aliyo yafanya waziri aliye pita, kwa
kuweza kuwapa polisi, uhuru ulio ptiliza, hadi inafikia hatua kwamba
wananchi wa maisha ya chini wananyimwa haki zao za msingi, na wenye pesa
ndio waliweza kupata haki zao na kuwakandamiza wale wasio kuwa nacho.
***
“Mume wangu utaweza, au ndio majukumu mazito uliyo kabidhiwa?”
Phidaya
alimuulimuuliza mumewe, huku akimfunga tai vizuri kwenda kwenye sherehe
ya wao kuapishwa inayo fanyikia kwenye viwanja vya ikulu muda wa jioni
ya siku hii,waliyo tangazwa kama mawaziri wapya.
“Mungu ni mwema nitaweza tu”
“Eddy mume wangu usije ukaenda ukaboronga huko ikawa ni mamatizo, mengine. Napenda tuishi kwa amani”
“Baby wewe ndio mtu wa kunipa mimi moyo, ila si mtu wa kunikatisha tamaa”
“Sio
kama nakukatisha tamaa mume wangu, kumbuka kwamba tumepitia shida
nyingi sana, hadi leo tumepata hii amani, ninaona kwamba tutaipoteza
amani hii”
“Never, nitahakikisha amani ya familia yangu kwanza, haiyumbi kisha nitahakikisha imani ya wananchi wangu, pia inapatikana”
“Sawa mume wangu mimi ninakuombea kila laheri, ila usisahau kwamba ninakupenda sana Eddy wangu, kupota maelezo”
“Nakupenda pia mke wangu”
Taratibu
Phidaya akambusu mume wake mdomoni, akamuweka vizuri koti la suti aliyo
ivaa. Wakatoka nje ya chumba chao na kuanza kushusha ngazi za gorofani
hadi wakafika sebleni, walipo wakuta Shamsa na Junio wakitazama tv.
“Badilisheni chaneli muda si mrefu mutaniona nikiwa nimetokelezea kwenye kideo, nitaringaje”
Eddy alizungumza huku akizunguka zunguka na kuwafanya watoto wake wote kucheka.
“Mungu wangu…!! Hapa hawajapata waziri”
Phidaya alizungumza huku akicheka kicheko, kilicho mfanya hadi machozi ya furaha kumwagika.
“Weee,
waziri wameupata, yaani varangati nitakalo kwenda kulianzisha ni kama
shehe aliye lishwa nguruwe pasipo kujua, sasa akagundua, hiyo movie yake
nitawaadisia nikirudi”
“Hembu nenda huko muda ujue unakwenda, ngoja uvuliwe huo uwaziri wako uone kama utazunguka zunguka tena”
“Nani anivue, subutuu nitampiga ngumii moja tuu, hadi aimbe haleluya”
“Dady usisahaku kuniletea zawadi?”
“Mwanangu, huko ikulu kuna zawadi gani”
“Eddy nenda bwana unachelewa, weee jizungushe zungushe kama tiara”
Eddy
akambusu mke wake, akafungua mlango na kutoka nje na kumkuta dereva wa
gari la serikali akiwa anamsubiria kwa ajili ya kumpeleka ikulu kwenye
sherehe hiyo.
“Shikamoo muheshimiwa?”
Eddy
hakuitikia salamu hiyo zaidi ya kuingia ndani ya gari na dereva huyo
naye akaingia ndani ya gari, akawasha gari taratibu wakatoka kwenye geti
kubwa la jumbu hili la Eddy alilo linunua siku chache baada ya kutoka
katika mapumziko ya harusi yao yeye na mke wake Phidaya.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment