Stori: AMRANI KAIMA, RISASI JUMAMOSI
SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa Salum ameweka wazi kutopendezwa na kitendo cha
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
kuendelea kuzaa nje ya ndoa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ akisema
kuwa ni kinyume na maadili na sheria za dini ya Kiislam.
Shehe Salum aliyasema hayo juzi Alhamisi
(Novemba 1, 2016) alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Global Publishers,
wachapishaji wa Magazeti ya Championi, Uwazi, Ijumaa Wikienda, Ijumaa,
Amani na Risasi zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar na kuzungumza na
waandishi pamoja na wafanyakazi wa idara nyingine.
Akijibu swali la Mwandishi Aziz Hashim
aliyetaka kujua dini inasemaje kuhusiana na watu kama Diamond kuendelea
kuzaa nje ya ndoa, shehe huyo alisema:
“Niseme tu kwamba hili si kwa Diamond na
Zari tu bali kwa wote wanaofanya zinaa. Dini ya Kiislam inaeleza kuwa,
kuzini ni dhambi. Hivyo kitendo cha Diamond kuendelea kuzaa nje ya ndoa
hatakuwa na tofauti na wanyama wengine ambao nao wanazaliana bila
kufunga ndoa.
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akiwa na waandishi wa habari na Global Publishers.
“Tofauti ya binadamu na wanyama kama
mbuzi, ng’ombe au nguruwe ni kwamba, sisi tunatakiwa kuzaliana baada ya
kufunga ndoa, kinyume chake tutakuwa tunapata dhambi.
“Halafu sasa tukio la kufunga ndoa wala
halichukui muda mwingi na halina gharama kubwa. Ni suala la wahusika
kumtafuta tu shehe, anakuja anatia ubani kisha mnaendelea na maisha
yenu. Kama ni kutumia pesa itakuwa ni elfu hamsini tu au laki moja.
“Labda niseme tu kwamba, hata mimi kama
kweli wamedhamiria kufunga ndoa, niko tayari kuwaozesha bure kabisa,
nitaweka gari yangu mafuta kuwafuata popote, wao wajipange tu wakiwa
tayari wanitafute.”
Shehe huyo aliongeza kuwa, anaona
litakuwa jambo jema kwa wawili hao kuoana kwani kuendelea kuzaa nje ya
ndoa ni kuwakosesha haki watoto wao hasa ile ya kurithi mali.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment