Loading...

Ray C Akubali Kujiuza!


    ray-c-kujiuza-8Na Waandishi wetu | Gazeti la Ijumaa Wikienda
DAR ES SALAAM: Kabang! Kufuatia kuwepo na madai kuwa, baadhi ya mastaa wamekuwa wakijirahisi kwa kuuza miili yao, kikozi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kiliingia kazini ili kupata ushahidi usiotia shaka juu ya skendo hiyo ambapo ilipewa baadhi ya majina ya mastaa Bongo ndipo ikaanza na mmoja baada ya mwingine.
Huku akiwa kwenye ubora wake akijiandaa kwa ujio wake mpya baada ya kuachana kabisa na matumizi ya madawa ya kulevya, OFM ilijikuta ikimuingiza mzimamzima’ katika mtego wake,  staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye kwa sasa yupo studio akipika vitu vikali huku jina lake la Kiuno Bila Mfupa likiwa limerejea.
ray-c-kujiuza-1Ray C akijibebisha kwa Kamanda wa OFM
MADAI YATUA OFM
Awali, kabla ya mchakato wa kumuingiza mkenge mrembo huyo mwenye historia ya kutikisa kwa muda mrefu na kibao chake cha Milele, OFM ilipokea madai kutoka kwa vyanzo vyake ambavyo vilidai kuwashuhudia mastaa mbalimbali wakijirahisisha kutokana na hali ngumu ya uchumi iliyopo kwa sasa.
“Kipindi hiki cha Magu (Rais Dk John Pombe Magufuli) ni noma. Mtonyo umekuwa adimu kwenye pochi za dada zetu. Walizoea kuishi maisha ya hali ya juu hususan wasanii. Sasa kwa kutaka waendelee kuwa juu, wamejikuta wakikubali kutongozwa na mwanaume yeyote ilimradi tu afike bei,” kilimwaga ubuyu chanzo.
OFM KIKAO CHA DHARURA
Baada ya kupata ubuyu huo, makachero wetu wa OFM, walikutana na kupanga mikakati ya kufanya jaribio kwa baadhi mastaa ambao wanatajwatajwa kuwa wanaingilika kirahisi.
Jumanne iliyopita, OFM wakiwa na orodha yao mkononi, waliamua kuanza baadhi yao akiwemo Ray C kwa kupata mahali pa kuanzia baada ya kudodosa kutoka vyanzo mbalimbali.
“Nendeni pale Mwenge kuna studio inaitwa Wanene, huwa anatinga pale. Naamini mkifika pale mtapata mwanga,”  alisema mmoja wa watu wa karibu wa Ray C.
ray-c-kujiuza-3…Wakiagiza vinywaji.
OFM YATUA WANENE
Makachero wetu wakiwa na vifaa maalum vya kunasa sauti na picha, walitia timu kwenye studio hiyo na kumkuta dada wa mapokezi ambaye alizungumza na mmoja wa OFM aliyejifanya anamhitaji Ray C kwa ajili ya tamasha.
OFM: Mimi namhitaji Ray C, nimeambiwa nikifika hapa naweza kumpata. Kimsingi mimi ni Mkurugenzi wa NGO yangu inayojishughulisha na mambo ya maendeleo vijijini. Sasa huwa nawatumia watu wenye majina ambao wamepitia changamoto mbalimbali kama hivi Ray C na ishu ya madawa ya kulevya kisha kuacha hivyo anakwenda kuzungumza ushuhuda wake kama elimu.
Dada Mapokezi: Kama ni suala la kazi haina shida ngoja nimpigie, si mnamlipa lakini?
ray-c-kujiuza-2OFM: Hela siyo tatizo kwetu.
Ndani ya dakika sifuri, Ray C kwa kutajiwa ‘dili’, aliibuka kwenye studio hiyo na haraka  mazungumzo ya ‘kibiashara’ yakaanza.
AKUBALI KWA SH. MIL 3
Mrembo huyo baada ya kusomeshwa kuhusu dili hilo, alikubali kufanya kazi kwa shilingi milioni 3 ambapo aliomba atanguliziwe shilingi milioni 1 na nusu kama ‘adavansi’ kwa makubaliano kwamba atakapofika mzigoni, atamaliziwa kiasi kilichobaki.
‘Kigogo wa NGO’ alikubaliana naye, akaahidi kumpa siku chache zijazo kisha kuagana na mrembo huyo baada ya kubadilishana namba za simu ambapo siku ya ahadi ya malipo hayo walikubaliana iwe Ijumaa (iliyopita) ili Jumamosi waondoke kwenda  Geita kupiga kazi.
ray-c-kujiuza-4‘KIGOGO’ AMBADILISHIA GIA
Katika kuthibitisha juu ya yale madai ya mastaa wengi huwa hawana hiyana katika suala zima la kupewa fedha ili watoe penzi, kesho yake (Jumatano iliyopita), kigogo huyo alimuomba Ray C amtoe mtoko wa chakula cha mchana, mtoto wa kike akasema hana neno!
Awali, Ray C alikubali kutanua na kigogo huyo katika moja ya Migahawa ya Mlimani City, Mwenge lakini baadaye mrembo huyo aliomba iwe Leaders Club, Kinondoni kwa sababu ya kukwepa macho ya watu.
LEADERS CLUB SASA
Baada ya kupanga miadi hiyo, Ray C ambaye alionesha kuwa na shauku na mtoko huo, bila kuchelewa alifika kwenye viunga vya Leaders Club akiwa ameambatana na mwanaume aliyemtambulisha kama ni mtu wake wa karibu ambaye anamtumia kusambaza kazi zake.
ray-c-kujiuza-5WAPIGA MISOSI, VINYWAJI
Kabla hata ya kibosile wa NGO hajafika, Ray C na msaidizi wake hawakuonesha kuwa na wasiwasi na kigogo huyo ambaye kwa muonekano alionekana ni mtu ambaye anachunika kirahisi huku ukizingatia alijitambulisha kuwa  hana uzoefu na Jiji la Dar.
KIGOGO ATUA LEADERS
Kigogo huyo alipofika, haraka Ray C alimtaka naye aagize chakula (huenda alionesha kumjali) ambapo kigogo huyo aliagiza maji huku mazungumzo ya hapa na pale yakichukua nafasi.
Baada ya mazungumzo mafupi, bosi huyo alilipa bili lakini akaomba mazungumzo ya faragha na Ray C hivyo yule msaidizi wa mrembo huyo akalazimika kuwaacha kidogo.
ray-c-kujiuza-6KIGOGO ASHUSHA ‘MADINI’
Huku makachero wakiwa wanaendelea kurekodi matukio yote, kigogo huyo alitumia fursa hiyo kumtongoza na kumwambia kwa kumueleza kuwa mbali na mambo ya tamasha lakini anamhitaji pia kimwili.
Somo lilimuingia mrembo huyo, akakubali lakini akaomba tendo hilo wasilifanyie Dar kwani wambeya ni wengi hivyo wamalize suala la tamasha na baada ya kumaliza, watalifanya suala hilo hukohuko Geita.
MUDA WA MAPICHAPICHA
Kuonesha kwamba somo lilimuingia Ray C, wakati anataka kuagana na kigogo huyo, walijikuta wapo kwenye ulimwengu mwingine wa kujiachia kwa kupigana ‘ma-selfie’ ya kutosha kwenye viwanja hivyo (tazama picha ukurasa wa mbele) kisha kuagana.
RAY C ANG’ANGANIA WALETI
Wakati wakiagana, Ray C alimuomba kigogo ampe fedha ya kukodia Bajaj lakini alipoambiwa na kigogo kwamba hakuwa na fedha ya kutosha, alimng’ang’ania na kuingiza mkono mfukoni ili achukue zilizopo.
“Mh! Wewe mkurugenzi bwana toa si hizi unazo!” alisikika Ray C.
Kigogo huyo alimpa shilingi 15, 000 kisha kuachana kwa staili ya ‘baby tutawasiliana baadaye’.
ray-c-kujiuza-7MAMBO YAIVA SASA
Ilipofika Alhamisi, mambo yakawa tofauti kabisa na walivyoanza. Safari hii kigogo akawa anamuita Ray C mke na Ray C naye akijibu mashambulizi kwa kumuita mume na akafikia hatua ya kuomba hela ya chai tofauti kabisa na yale mazungumzo ya tamasha. Cheki moja ya meseji yao ya kimalovee:
Kigogo: Niambie mke wangu.
Ray C: Niambie mume wangu wa Kisukuma.
ATUMIWA ‘TWENTI’ YA CHAI
Wakati wawili hao wakizidi kuzama kwenye dimbwi la malovee, ilipofika Ijumaa, kigogo alimtumia Ray C shilingi elfu ishirini ya chai na kumuomba radhi kwa kuchelewa kuituma kutokana na ubize wa majukumu yake lakini mrembo huyo aliipokea kishingo upande akidai amemkwaza.
ATANGAZA DAU
Ili kumaliza kazi yake ya kiuchunguzi, kigogo aliempigia simu Ray C na kumweleza kwamba anamhitaji kulala naye usiku mmoja katika hoteli moja iliyoko wilayani Temeke na yuko tayari kutoa kiasi chochote cha fedha.
Bibie akakubali kuwa yupo tayari kulala naye kwa shilingi milioni moja lakini akaomba fedha hiyo apewe kabla hajaingia kwenye hoteli hiyo maana ameanza kupoteza imani naye hususan baada ya kumcheleweshea fedha   ya chai.
“Nikikute changu mapokezi ndiyo niingie maana nawe sikuamini,” alisikika Ray C.
Kwa kuendelea kukosa imani, baadaye Ray C alisema kama si kuikuta fedha hiyo mapokezi basi amtume mtu na akishampa ndiyo yeye atakwenda mahali alipo kigogo huyo.
OFM YAMALIZA KAZI
Kwa kuwa lengo lilikuwa ni kuona kama Ray C anakubali kujiuza, OFM iliishia hapo baada ya bibie kukubali na OFM ikamchana kwamba ilikuwa kazini.
ATAKIWA KUWA MAKINI
Kufuatia ishu hiyo, OFM imempa ushauri Ray C ambaye amerejea kwenye gemu na kuachana na madawa ya kulevya kuwa awe makini na kwamba si kila mtu atakayemhitaji kikazi atakuwa na lengo hilo bali wengine wanaweza kuwa ni walewale wa kumuingiza kwenye majanga kama ilivyokuwa awali hivyo achukue tahadhari kubwa.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright KISWAGA BLOG
Back To Top