Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitaja
rushwa kama changamoto sugu ambayo bado inaendelea kulitafuna taifa la
Tanzania katika miaka yake 55 ya Uhuru.
Rais
Magufuli ameitaja changamoto hiyo leo akati akiwaongoza watanzania
katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara ikiwa ni mara
ya kwanza tangu aingie madarakani na kutaja changamoto nyingine kuwa ni
tatizo la ajira pamoja na umasikini.
Akizungumza
katika hotuba yake ya shukrani katika maadhimisho hayo ambayo
yamefanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli,
amesema kuwa serikali yake itaendelea kupambana na vitendo na rushwa na
ufisadi, kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo.
Aidha
Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa serikali itahikisha kuwa inaondoa
uonevu hasa kwa wananchi wanyonge ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto
zinazowakabili ili kila mtanzania aweze kufaidika na matunda ya nchi
yake.
Maadhimisho
hayo ambayo kwa mujibu wa Rais Magufuli ndio ya mwisho kufanyika Jijini
Dar es Salaam na kuanzia mwakani yataadhimishwa Dodoma, yamehudhuriwa
na viongozi mbalimbali wastaafu na serikali pamoja na mabalozi wa nchi
mbalimbali zenye uwakilishi hapa nchini.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment