sanchoka-7Akifanya mahojiano (Exclusive Interview) na Channel maarufu hapa mjini ya Global TV Online, Sanchoka amefunguka kuwa uhusiano wake na Idris ulianzia kwenye Apartment wakati walipokuwa wamekwenda Afrika Kusini (Sauzi) kushuhudia utoaji wa Tuzo za MTV Africa (Mama) hivi karibuni.
“Mimi na rafiki zangu tulipanga kwenda kushuhudia MTV Awards huko Sauzi, bahati mbaya apartment tuliyofikia ndipo alipokuwa amefikia Idris pia.”
“Tulikuwa watu wengi kwenye hiyo apartment, walikuwepo wakina Shilole, na wengine wengi,”
Akanusha kuhusu kuwa wapenzi
Licha ya kuelezea kinagaubaga alivyokutana na Idris, Sanchoka amekanusha kuhusu taarifa zinazosambaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mshindi huyo wa BBA 2014.
“Idris alikuwa ana-anounce (anatangaza) awards, kwa kuwa alikuwa VIP kule mbele, alinifuata na kuniomba niwe partner wake ili twende nikakae naye kule mbele, haikuwa urafiki wa mapenzi bali ulikuwa urafiki wa kawaida tu.” Ameeleza Sanchoka ndani ya Studio za Global TV.
Amfungukia Gigy Money
Mbali na kufunguka alivyokutana na Idris, Sauz amefunguka pia kuhusu uhusiano wake na modo mwenzake ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM, Gigy Money ambaye alidaiwa kutoka kimapenzi na Idris huyo huyo.
sanchoka-8“Uhusiano wao (Idris na Gigy) mimi haujani-affect chochote kwa kuwa mimi na Idris tulikuwa marafiki wa kawaida tu, na hatujawahi kuzungumzia kuwa na uhusiano wa kimapenzi”. Alisema Sanchoka.
Pia Sanchoka ameeleza kuwa yeye kwa sasa ana mchumba wake mbali na huyo wanayemsema mitandaoni (Idris), licha ya kutobainisha iwapo atafanya taratibu za kufunga naye ndoa siku za hivi karibuni.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment