Kauli hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro jana alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatolea ufafanuzi leo.
Mzee wa Upako: Wote Walionichafua Watakufa Mwakani, Wasipokufa Nitaanza Kuuza Gongo
“Anasema hao waandishi watakufa kabla ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni suala zito, tumeandaa mkutano na waandishi wa habari tutalizungumzia suala hilo kesho (leo),” alisema Kamanda Sirro.
Katika kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi aliyemuandika vibaya ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama wataendelea kuishi, ataacha kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza gongo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment