![15073351_1211637858928457_1027844742407885980_n](https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2016/12/15073351_1211637858928457_1027844742407885980_n.jpg)
Kuelekea kule tunapotaka kuwa hatuwezi kufika ghafla kwani ni safari ndefu ambayo itatutaka tuvae nguo na viatu kisha twende kituoni kusubiri mabasi.
Tanzania tulianza kama watoto ila tukaanza kukua na kukua na leo hii tupo hapa tukiongozwa na mtu mwingine, Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli.
Hatuwezi kuponda kwa kila kitu, wakati mwingine wewe kama Mtanzania ni lazima uonyeshe uzalendo, kama unavyosema vibaya vitu vinapokuwa ndivyo sivyo basi pongeza pale vinapofanyika vizuri kumtia moyo aliyevifanya.
Usisubiri Mkenya aje aisifie Tanzania, usisubiri Mganda aje aisifie….heshima na sifa zinatakiwa zianze kwako kwanza kabla ya watu wa nje.
Nampongeza Magufuli, amefanya kazi nzuri na sisi Watanzania tupo nyuma yake, tutamsapoti kwa moyo kwa sababu Mungu alitaka tuzaliwe Tanzania kwa makusudi yake na ndio maana hakutaka uzaliwe Sudan, Malawi na nchi nyingine.
Najivunia TANZANIA yangu…Najivunia Rais wangu.
E.J SHIGONGO
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment