Siku mbili baada ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Tiba na Magonjwa ya Binadamu
(NIMR), Dk Mwele Malecela, mwanasayansi huyo amesema yupo imara na
atazungumza wakati muafaka ukifika.
“Kwa leo siwezi kuzungumza lolote kutokana na hali ilivyo, na namna
jinsi watu wanavyoendelea kulizungumzia jambo hili lakini nitazungumza
wakati ukifika na mtajua,” alisema
Dk Mwele kwa sauti ya uchangamfu.
Uteuzi wake ulitenguliwa Ijumaa usiku baada ya kutoa ripoti ya mwaka ya
taasisi hiyo iliyoonyesha kuwa watu 80 waliofanyiwa utafiti
waligundulika kuwa na virusi vya homa ya zika.
Taarifa ya utafiti huo ilionyesha kuwa kati ya watu 533 waliopimwa, 83
(asilimia15.6) walikuwa wameambukizwa virusi vya homa zika. Pia, kati ya
watoto wachanga 80 waliozaliwa na ulemavu wa aina mbalimbali, asilimia
43.8 walikuwa wameambukizwa virusi vya homa ya zika.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
Post a Comment