Jumapili ya December 18 2016 KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana
Samatta iliwakaribisha Standard de Liege katika uwanja wao wa Luminus
kucheza mchezo wao wa 18 wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2016/2017.
Genk wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani walianza kupata goli la
uongozi dakika ya 3 kupitia Omar Colley kabla ya dakika ya 16 Orlando
Carlos kufunga goli la kusawazisha na dakika ya 25 Ishak Belfodil
kuongeza goli la pili na kuanza kuwa makini na ulinzi wa goli lao
kuwadhibiti Genk.
Mchezo ulienda mapumziko KRC Genk wakiwa nyuma kwa goli 2-1 hali ambayo
iliwawia vigumu kupata goli la kusawazisha mapema, Samatta ndio alikuwa
mkombozi wa KRC Genk baada ya dakika ya 77 kupachika goli la kusawazisha
kwa kichwa kupitia krosi iliyopigwa na Jere Uronen na kuufanya mchezo
kumalizika kwa sare ya 2-2.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
Post a Comment