Bondia Mtanzania Francis Cheka ambaye mwishoni mwa wiki alipoteza
pambano lake nchini India alilopigana na raia wa nchi hiyo Vijender
Singh, ameibuka na kusema kuwa mpinzani wake huyo hakumpiga, ila
alibebwa na mwamuzi.
Akiongea katika kipindi cha 5Sports cha EATV kwa njia wa simu kutoka
nchini India, Cheka amesema katika raundi hiyo ya tatu, alipata tatizo
katika kifaa chake cha kulinda meno kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na
kikohozi, na wakati anakifanyia marekebisho, ndipo mwmuzi akatangaza
mshindi, bila kumuuliza Cheka mwenyewe kama alikuwa anaendelea au la.
“Tatizo nilikuwa nakohoa, nilijiandaa vizuri kumpiga yule Vijender,” alisema Cheka.
Pia katika mtandao wake wa Instagram aliandika:
Pale ambapo matokeo yamepangwa, tunaenda kukamilisha ratiba tu, Refa
unaona mouth guard imetoka na unaendelea kuchezesha… Watanzania nadhani
mmeona, tusiwage wanyonge kwao na kwetu pia… Nadhani nimeliwakilisha
taifa vyema, kuitangaza Morogoro, Tanzania, Kiswahili na Kimakonde pia.
VIDEO:
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
Post a Comment