Lakini baadaye kila mmoja aliendelea na maisha yake ikiwemo Petit kumuoa dada yake Diamond, anayejulikana kama Esma. Lakini siku za hivi karibuni, wawili hao wameonekana kuwa karibu tena kiasi cha kuwafanya watu wahisi wamerudiana. Kajala amelazimika kuzizungumzia tetesi hizo na kukanusha kurudiana na ex wake huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo Kajala ameandika:
"Jamani i think this is too much sasa na mnavuka mipaka. ifike muda watu muwe mnatumia akili kufikiria mnavyotaka kusema. Hivi kama ulishakuaga na mahusiano na mtu na hayo mahusiano yakaisha So huruhusiwi kuongea nae?? Are you guys Owkay?? Hivi mnajua mchango wa Petit katika maisha yangu? Mnajua jinsi alivyonisaidia wakati niko katika kipindi kigumu cha jela? Au mnakua mnaongea tu ili mfurahishe watu... Petit sasahivi ni part ya familia yangu na sio mambo ya mapenzi. Kwani mimi sijui kama ana mke na ana familia? Why watu mnakua na akili fupi sana za kufikiri....mimi siwezi kuwa na ugomvi na esma kwasababu ya petit...esma ni mke wake na wana mtoto na kila mtu anajua...na mimi nitaendelea kumchukulia petit kama ndugu na rafiki wa karibu kwasababu ya mchango na msaada wake katika maisha yangu. Sitoacha kuongea na petit kwa ajili ya ujinga wenu mnaosema...haitawahi kuja kutokea...sasa basi, i think am clear na tumeelewana kabisa...nyie ndo mnakuaga chanzo cha watu kugombana bila sababu..tafuteni kazi za kufanya... have a lovely evening"
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment