Watu walizungumza mambo mengi sana baada ya kusikia kuwa Harmonize na Jackline Wolper na uhusiano wa kimapenzi huku walio wengi wakiamini kuwa alikuwa akitafuta kiki tu. Walioamini hivyo ni kutokana na uhusiano wa kimapenzi ambao uliwahi kuwapo kati ya Diamond Platnumz ambaye sasa ni bosi wa Harmonize na Wolper.
Katika mahojiano haya yaliyofanyika kipindi cha nyuma kati ya Zamaradi Mketema wa Clouds Tv na mwanamuziki Diamond Platnumz, Diamond alikiri kuwa aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wolper na pia aliandika wimbo wa Mawazo baada ya kuumizwa na msichana huyo.
Mbali na Wolper, Diamond amekiri kuwa aliwahi kuandika nyimbo nyingi kuhusu Wema Sepetu ambaye alikuwa ni mmoja wa watu aliowahi kuwapenda sana lakini wakamuumiza.
Swali ambalo limekuwa likiwatatiza wengi hadi leo, ni kwanini Diamond alimuacha Harmonize kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Wolper kama yeye alishawahi kutoka naye, tena akaishia kumuumiza?
Hapa chini ni video ya Diamond Platnumz na
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment