MWANZA: BIBI mmoja aliyejulikana kwa jina la Amina Hamisi (56) mkazi wa
Mtaa wa Mahina, Kata ya Butimba, Jijini Mwanza, anashikiliwa na Jeshi la
Polisi mkoani humo baada ya kumlazimisha mjukuu wake Rehema Sadiki (7)
kula kinyesi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi
Augustino Senga amedai kuwa tukio hilo limetokea Novemba 11, mwaka huu
ambapo mtoto huyo alikwenda chooni kujisaidia na kushindwa kumwagia maji
ili kuondoa kinyesi chake ndipo bibi yake ili kumuadhibu alimuamuru
kula kinyesi hicho kitendo ambacho mtoto huyo alikitekeleza.
Baada ya tukio hilo kutokea raia wema walitoa taarifa polisi ambao
walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.
Kamanda Senga ametoa wito kwa wakazi wa jiii la Mwanza kutoa ushirikiano
kwa jeshi la polisi ili kudhibiti vitendo vya kikatili hasa kwa watoto
wadogo na kuongeza kuwa ukatili ni kosa kisheria hivyo wananchi waache
kufanya vitendo hivyo na watakao bainika sheria itachukua mkondo wake.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
Post a Comment