Loading...

YALIYOJIRI Mwanza Mjini: RC, DC na CD Wataweza Kukalia Ofisi zao na Kutoa Maamuzi na Kueleweka?

FM Radio zote za jijini Mwanza sasa hivi ni mjadala wa maamuzi ya Rais na zinawekwa Clip za matamko ya Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya Nyamagana na Mkurugenzi (CD) wa jiji kuhusu suala la wamachinga waliyotoa siku zilizopita kuhusu suala hilo na kuonekana kuwa walikuwa tofauti kabisa na hiki alichosema Rais.

Hata mbunge wa Nyamagana alipohojiwa amepata nafasi ya kuwaruka kabisa viongozi hao kiasi cha kuonyesha maamuzi yao yalikuwa yao pekee kwa nia ya kukomoa Wamachinga na mama ntilie.

Hii ni fedheha kubwa sana kwa wateule hao wa kisiasa na kiutendaji na wanakosa kabisa sifa ya kuendelea kuwaongoza watu wa Mwanza kwa siku zijazo kwani hawawezi tena kuwa na maamuzi ambayo yatakuwa yamesimama bila kudharauliwa.

Je, wataamua wenyewe kujiuzulu ili kulinda heshima zao au watataka waendelee kufanya kazi kama picha tuu? Maana kila anayehojiwa mtaani anawaponda na kuwadharau kuwa kazi imewashinda ndio maana aliyewateua kaamua kuifanya mwenyewe.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright KISWAGA BLOG
Back To Top