Wakina dada hao ni Savita (23), Monisha (18) na Savitri Sangli (16) ambao wanaishi katika kijiji cha Pune, India na wamerithi kwa baba yao uotaji nywele huo mwili mzima.
Wataalamu wanasema kuota nywele mwili mzima yaani hata kwenye sehemu ambazo hazipaswi kuota nywele ni ugonjwa ambao kitaalamu unafahamika kama ‘Werewolf Syndrome’ ambapo seli hubadilisha mfumo na kuzifanya nywele kuota sehemu zote mwili na ni ugonjwa wakurithi.
Na kwa wasichana hao wamekuwa wakiota nywele kwa haraka sana na nyingi mwili mzima, wana ndevu lakini pia puani kwenya paji la uso na sehemu nyingine nyingi, jambo ambalo linawafanya waonekane tofauti na wasichana wengine na wengi huwashangaa na wakati mwingi huwabeza.
Hali hii imezima kabisa ndoto zao kwani wanajiona tofauti na hivyo wanaamini hawataweza kupata mambo muhimu kama wanawake wengine kama vile kuolewa, kuajiriwa, kujiremba na hata kuvaa nguo kawaida kama ilivyo kwa wanawake wengine.
Na hii inawaumiza sana kwani kwa tamaduni za kijiji chao ikiwa umefikia umri wakuolewa na ukasalia nyumbani inahesabika kama mkosi kwa mtu binafsi, familia na kijiji kwa ujumla wake.
“Wanangu hawa watatu wananisononesha sana kwani hali yao inawanyima raha na wanatafuta njia yoyote yakuwasaidia kuziondoa nywele hizo ili wawe kama wasichana wengine. Gharama yakufanya ‘surgery’ kwa kila msichana zinahitajika dola za kimarekani 7000 ambazo ni sawa na shilingi 15,250,200 za kitanzania, hivyoi jumla zinahitajika shilingi milioni 45,750,600. Na kwa bahati mbaya sina hizo pesa,” alisema mama wa watoto hao
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment