Idara
ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imewakamata wasichana 13 kutoka nchi
za Nebal na India wenye umri kati ya miaka 18 na 26 ambao wameletwa
nchini kinyume cha sheria na kuendesha biashara ya ukahaba katika jijini
humo.
Akiongea
na waandishi wa habari leo mara baada ya kufanya oparesheni ya kufunga
madanguro yote na kuwasaka raia wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha
Sheria, Kamishna wa Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule amesema
mbali na raia hao wa kigeni pia wamewamakata raia wa Kitanzania mbao wanashirikiana na wahamiaji hao.
Amemtaja
Bwana Mohamed Shabani Magamba ambaye anatengeneza vibali vya kugushi
ambapo pia amekutwa na pastpoti 4 za raia wa nchi za Nigeria, Botswana,
Somalia na Uingereza.
Bwana
Msumule ameitaja Wilaya ya Kinondoni kuwa inaongoza kwa kuwa na
Madanguro ikifuatiwa na Temeke ambapo kwa sasa wanajipanga kuyaondoa kwa
muda wa siku 10 madanguro hayo pamoja na kuendesha oparesheni kubwa
katika Mitaa ya Msimbazi, Lumumba na Uhuru katika soko la Kariakoo na
maeneo ya Mtoni Mtongani na Sabasaba ambako wamekwisha yafanyia
uchunguzi wa kina.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment