Hili
ni tukio pale wanandoa waliponaswa wakifanya mapenzi mchana kweupe
ufukweni tena mbele ya wazazi na watoto waliobaki wamepigwa butwaa na
kushindwa kuamini macho yao.
Simon
Cummins ambaye alikerwa na tukio hilo amesema kuwa yeye na rafiki zake
walikuwa wakistarehe ndipo waliposikia kelele za mwanamke aliyekuwa
akilalamika kimahaba huku akitembea kando ya ufukwe wa Brighton.
Cummins,
mwenye miaka 30, alikwenda kwenye sherehe ya rafiki yake usiku mmoja
kabla lakini aliamka Saa 3 asubuhi kufuata gari lake kwenda kutazama
mechi ya soka ya hisani, ndipo aliposhuhudia 'uchafu' huo.
Hatahivyo,
wakati sherehe ikiendelea kwenye eneo maarufu la Gati ya Brighton,
walisema walisikia kwanza kisha kuona, mwanamke mwenye nywele nyekundu
akiwa juu ya mwanaume ufukweni.
Hatua
chache kutoka eneo la tukio, watu waliokuwa mapumzikoni na watoto
walionekana wakikatiza kando ya wanandoa hao ambao hawakuonesha kujali.
Wakati fulani mtoto mmoja aliwanyooshea kidole wanandoa hao kabla ya
mama yake aliyekereka kumwondoa hapo.
Tukio hilo limetokea karibu na gati upande unaotumiwa na watu kwenye ufukwe wa Brighton.
"Ilikuwa ni kama uasherati au siku za mwisho za Roma. Ilikuwa sehemu ya kutisha kuweza kutazama."
Cummins alisema kuna wakati wanaume kadhaa waliwafuata wanandoa wale na mmoja wao alijaribu kushiriki nao.
Polisi wa Sussex walisema waliwafuata wanandoa hao na kuwakamata kabla ya kuwalipisha faini ya papo kwa hapo.
Lakini Simon anayetokea Waltham Abbey, mjini Essex, alisema wanandoa hao walitakiwa kuwekwa mahabusu.
Alisema:
"Ilikuwa ni mchana kweupe, familia zilizokuwa karibu zilikuwa umbali wa
mita 10 tu kutoka pale, kuliwa na watoto wakicheza karibu. Ilikuwa
inakera mno.
"Nina wapwa zangu na wadogo zao na kama ningeona kitu kama kile kinaendelea mbele yao ningekuwa na cha kusema.
"Mwanaume
na mwanamke hawakuwa wakionekana kama wamevuta dawa za kulevya,
walionekana kama watu wengine wa kawaida, japo walionekana wakifanya
ngono mchana.
Cummins
ambaye alikuwa na rafiki zake Ben Stone na Richard Jones, alisema
sababu ya wao watatu kugundua wanandoa hao walikuwa wakifanya jambo
lisilo la kawaida ni sababu mwanamke alikuwa akipiga kelele za
'kimahaba'.
Msemaji wa polisi wa Essex alithibitisha kwamba maofisa walikwenda eneo la tukio Jumapili.
Alisema:
"Polisi waliitwa kwenye ufukwe wa Brighton, karibu na West Street,
Jumapili iliyopita pale iliporipotiwa kwamba wanandoa wawili walikuwa
wakifanya mapenzi.
"Wawili hao walikamatwa na kutozwa faini."
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment