Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amefunguka kwa kusema kuwa moja ya sababu ambayo ilimfanya apotee kwenye muziki ni kitendo cha kuachana na meneja wake.
saida-karoli
Muimbaji huyo ambaye aliachana na meneja wake toka 2007, amedai kitendo hicho kilimfanya ashindwe kujisimamia na kumfanya ashuke kwenye muziki.
“Baada ya kuachana na meneja wangu sikuweza kujisimamia mimi mwenyewe na pia kwa wakati ule ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu muziki una mambo mengi na mimi nimekulia kijijini kwahiyo kujua baadhi ya vitu ilikuwa ngumu sana,” Saida aliiambia BBC.
“Sina nilipo kosea lakini najua kila kitu chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho, simaanishi huo ndo mwisho wangu ila kwa kuwa nilianza na mtu, sasa unapomalizana naye ni kama unaanza maisha mapya ndio kitu kilicho nitokea mimi,” aliongeza.
Pia muimbaji huyo amesema kwa sasa anajipanga kuja kwa kishindo na kufanya mapinduzi katika muziki wa asili nchini.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment