MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
"Yes mpango umekwenda vizuri kama nilivyo panga"
John
alionekana akiwa amefurahi sana kwa habari hiyo. Iliyo onyeshwa kwenye
kituo hichi cha habari. Hii ni baada ya muandishi huyo kudai kwamba
ndege hiyo ilikuwa ikitokea nchini Brazili, kwenda bara la Afrika.
Abiria wote waliomo ndani ya ndege hiyo wamekufa kwenye mlipuko huo wa
ndege ulio tokea majira ya mida hii ya mchana, jambo lililo nipa
wasiwasi mwingi, hadi nikajihisi mwili mzima kuishiwa na nguvu.
ENDELEA
Pretty akamtazama John kwa umakini huku akionekana kuwa na mshangao mkubwa.
"Unafurahia nini?"
"Kuna mpango niliupanga na vijana wangu, kuhusiana hiyo ndege"
"Unataka kusema wewe umehusika kwenye mpango wa hiyo ndege kulipuka?"
Pretty
alimuuliza John huku akimkodolea macho ya wasiwasi. Mimi hata nguvu ya
kunyanyuka kwenye kochi sikuwa nayo hii yote ni kwakuiwazia familia
yangu.
"Ndio"
"Kwanini?"
Kuna mjinga nilimuua, sasa ulikua muda wakuiteketeza famia yake"
Nikastukia
kumuona Pretty akinyanyuka kwa hasira na kumrukia John, hadi sofa alilo
likalia wakaaanguka nalo. Sheila akasimama kwa haraka na kumchomoa
Pretty aliyekuwa akimshambulia mumewe kwa kumpiga kwa makofi mfululizo.
"Wewe ni gaidi"
Pretty alizungumza kwa hasira, huku mimi nikiwa nimepigwa na bumbuazi lililo nifanya nishindwe kufanya kitu cha aina yoyote.
"No no nakudanganya Pretty"
John alizungumza huku akicheka.
"Muongo wewe"
"Kweli Pretty siwezi kufanya kitu kama hicho. Kwanza nitaanzia wapi. Eti Henry kweli ninaweza kufanya jambo hili?"
Nilitabasamu
tu, hata kinywa changu kikashindwa kufunguka. Tangu nizaliwe sijawahi
kukumbana na hali ya mshangao kama hii, iliyo nimaliza nguvu zote.
Pretty
akafungua mlango na kutoka huku akiubamiza kwanguvu. Jambo lililo
nistua na kurudi kwenye hali yangu yakawaida. Nikanyanyuka kwa haraka na
kumfwata Pretty ndani kwake
"Nilazima nimpeleke polisi nikamstaki"
Pretty alizungumza kwa hasira huku akiingia chumbani kwake. Nikamfwata na kumkuta akiwa amekaa kwenye kitanda huku akilia.
"Pretty nisikilize, kitu kimoja"
"Nahitaji zile video mbili kama una flash zihifadhi sawa"
Pretty
alibaki akiwa amenikodolea macho. Nikatoa simu mfukoni na kuingiza
namba za Blanka. Ikaita kwa muda mrefu, kisha ilapokelewa.
"Blanka wamefika?"
"Hawajafika"
Jibu
la Blanka likanifanya nizidi kuchanganyiliwa, hadi mwili ukawa
unanitetemeka kwa woga kwani swala la akufiwa nafamilia tena kwa wakati
mmoja, sikuliwazia kichwani mwangu.
"Hawajakupigia?"
"Hapana hawajanipigia"
Nikakata
simu nakushusha pumzi kubwa, nikabaki nimesimma pasipo kuzungumza kitu
chochote na Pretty. Nikamshika mkono Pretty na kumnyanyua juu.
"Twende kwangu"
"Kufanya nini?"
"Twende tu"
Tukatoka sebleni, Petty akaziingiza video zote mbili kwenye flash, kisha akachukua begi lake lenye laptop.
Tukaondo
hadi nyumbani mwangu. Kitu cha kwanza nikaifwata simu ya chumbani
kwangu. Nikamiinya kitufe cha kusikiliza ujumbe wa sauti, ili kutambua
kama kuna ujumbe wowote wa suti ulio ingia nikiwa sipo.
"Eddy mume wangu, mbona hupokei simu?"
Ilikuwa nisauti ya Phidaya, kwenye ujumbe wa kwanza wasauti
"Tumeamua
kubadilisha safari, tupo Marekani kwa sasa. Shamsa ndio alitoa
pendekezo la sisi kubadilisha safari. Ukipata ujumbe huu usiwe na
wasiwasi, tupo salama na kesho tunakwenda Tanzania. Nakuupenda mume
wangu"
Ujumbe
wasauti, ukawa umekwisha. Nikashusha pumzi nyingi, huku tabasamu pana
likiwa usoni mwangu. Nikatoka sebleni na kumkuta Pretty akiwa anaminya
minya batani za laptop yake.
"Unafanya nini?"
"Nachapisha habari za kumchafua John kwenye mtandao na kuituma hii video ya mauaji"
"Hapana usifanye hivyo"
"Kwanini?"
"Nataka kumuua John taratibu"
"Kumuua taratibu!?"
"Ndio"
Nikaanza kumuadisia historia nzima ya maisha yangu. Kuanzia nilivyokua shule na John hadi leo ni adui yangu.
"Sasa kwanini hutaki tumuue sasa hivi?"
"Pretty mpango wangu ni mrahisi sana. Nataka kumuua kwa kifo chakumzalilisha na kumtesa sana."
"Ila familia yangu ipo salama"
"Kweli?"
"Ndio"
Pretty akanikumbatia kwa furaha, huku machozi yakimwagika kwani historia yangu ilimuuzunisha sana.
Siku
ya pili, tukakutana na John na Sheila wakiwa kwenye maandalizi.
Ikamlazimu Pretty kuwaomba msamaha kwa kile kilicho jitokeza jana
mchana. Hii ikiwa ni moja ya mpango wetu wa kumteketeza John na Sheila,
pasipo wao kujua chochote.
"Nilijua tu nihasira, mimi nimemsamehe"
John alizungumza huku akimpa mkono Pretty.
Ikawa
ni furaha kubwa sana kwa John, na Sheila wake. Wakiamini urafiki wetu
utaendelea kama kawaida na laiti wangejua wasinge ruhusu kujipendekeza
kwetu.
***
Siku ya harusi ya John ikawadia, mimi na Pretty tukawa nimiongoni mwa
waalikwa kwenye sherehe hii ndani ya kanisa hili kubwa la Roman katolic.
"Kila kitu umekipanga sawa?"
Nilimuuliza
Pretty mara baada ya kufika kanisani, tukishuka kwenye gari yetu aina
ya BMW, tulilo linunua jana kwa kazi moja tu iliyopo mbele yetu.
"Kila kitu kipo powa mpenzi"
Kabla sijazunguza chochote simu yangu ikaita kwa namba ya Blanka, ndio inayo nipigia.
"Nipigie bwana"
Blanka alizungumza kwa furaha, ikanibidi nikate simu na kumpigia.
"Ndio kaka Eddy. Kweli wewe nikiboko"
"Kwanin?"
"Yaaani toto lako nikopi na wewe yaani umefanya kazi kubwa kulitafuta"
"Kwani wamefika?"
"Ahaaa ndio nipo hapa uwanja wa ndege nimewapokea yaani weee acha tuu. Ninafuraha yakufa mtu"
"Hembu mpe Junio simu nizungumze naye"
"Dady tumefika Tanzania"
"Umemuona antie?"
"Ndio, ila kuna joto kali"
"Poleni mwanangu, mpe mama simu"
Nikasikia
sauti ya Junio ikimuita Phidaya, furaha ikazidi kuongezeka moyoni
mwangu, nakujiamini zaidi kwamba kazi yangu inazidi kuwa nyepesi zaidi.
"Mume"
"Niambie mke wangu"
"Safi, tumesha fika Tz yaani hapa nijoto"
"Sasa hivi nisangapi?"
"Saa.....saa tano inakwenda saa sita usiku"
"Poleni kwa uchovu"
"YĆ ani wee acha tu, yaani tumetoka Marekani jana alfajiri, tunashukuru Mungu ndege tuliyo panda haikupita kwenye nchi nyingi"
"Ilikuwaje mukaenda Marekani?"
"Hilo swali muulize mwanao Shamsa"
"Mpe simu"
"Vipi wewe"
"Ahaaa safi baba"
"Hembu sogea pembeni uniambie nini kilitokea?"
"Wee
acha baba, kipindi tupo uwanja wa ndege kuna jamaa nilikua ninamtilia
mashaka, sasa tulipo maliza kukaguliwa. Kipindi sasa tunaelekea kupanda
basi lile linalo wapeleka watu kwenye ndege"
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment