Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
ILIPOISHIA
“Nafanya hii, kwa ajili yakulipiza kisasi cha mume wangu”
“Ngoja kwanza, nipo tayari kufa, ila ninakuomba usimuue mke wangu”
Nilizungumza
kwa ujasiri, nikiwa nipo tayari kwa kufa, Madam Mery akalinyanyua panga
lake juu, akalishusha kwa kasi kwenye mkono wangu wa kulia
ENDELEA
Nikatoa
ukulele mkali, ulio mfanya madam Mery kusitisha zoezi lake kuukata
mkono wangu, panga lake likiwa limesimama sentimita chache kutoka ulipo
mkono wangu
“Madam, ninakuomba unisamee”
Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagika usoni mwangu, madam Mery akanitazama kwa macho ya hasira yaliyo jaa
ukatili mkubwa, akawatazama Victoria na John ambao macho yao yote yalikuwa kwetu
“Natambua
kwamba mimi nimkosaji sana kwako, ninastahili kufa mbele yako, ila si
mbele ya macho ya mke wangu.Mtazame jinsi alivyo katika hali yake.Mule
ndani amebeba kiumbe kama ulicho kuwa umekibeba wewe, miezi tisa, na
Derick akakiangamiza mbele yetu.Yule ni mwanamke mwenzako ambaye
anauchungu kama wewe”
Nilizungumza
huku machozi yakiendelea kunimwagilka usoni mwangu, madam Mery kwa
mbali machozi yakaanza kumlenga lenga, macho yake yamebadilika rangi na
kuwa mekundu kiasi huku sura yake ikiwa imejaa mikunjo kwenye paji lake
la uso akinitazama kwa uchungu sana
“Mery
mimi pia ni binadamu, kumbuka ni mambo mangapi tuliyafanya tukiwa
pamoja, vuta kumbukumbu ni vitu vingapi tulishiriki tukiwa pamoja,
Eheeee, leo hii unataka kuimwaga damu yangu, leo hii unataka kunisulubu
kikatili, le……..”
“Eddy STOP TALKING”(Eddy nyamazakuzungumza)
Madam
Merry alizungumza kwa sauti ya juu, yenye uchungu ndani yake.Akalitupa
chini panga lake alilokuwa amelishika.Machozi mengi yakaanza kumbubujika
usoni mwake, John na Vivtoria wakabaki wakimtazama madam Mery, ambaye
taratibu alianza kupiga hatua za kuelekea kwenye gari lake alilo kuja
nalo
“Madam Vipi?”
John alizungumza huku akimwafwata madam Mery kwa nyuma
“John ninakuomba uniache”
Madam Mery aluzungumza huku akiunyanyua mkono wake mmoja akimzuia John asimfwae anapo elekea
“Ila madam haya sio makubaliano yetu”
“John sipo sawa nimekuambia usinifwate”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya ukali, huku machozi yakiendelea kumchuruzika usoni mwake.
“Sasa Madam tumfanye nini Eddy?”
Madam
Mery akageuka kwa hasira, hadi John akastuka kidogo, akanitazama jinsi
machozi yanavyo nimwagika, akayafumba macho yake kwa sekunde kadhaa,
akionekana akifikiria kitu cha kufanya juu yangu.
“Kesho nimkute akiwa hai”
Madam
Mery alizungumza kwa sauti ya upole, kisha akaelekea lilipo gari lake,
akafunguliwa mlango na mlinzi wake, akaingia ndani ya gari na wakaondoka
zao.John akalisindikiza magari ya Madam Merry yanayotoka kwenye geti
kubwa la Godauni, lilipo fungwa taratibu John akanigeukia, akanitazama
kwa macho ya dharau huku Victoria akiwa amejichokea, kwani ninaamini
mipango yao waliyo kuwa wameipanga dhidi yangu imeharibika.John
akamfwata Victoria sehemu alipo simama, wakanong’onezana kwa muda kasha
wakamtama Phidaya ambaye muda wote, amejilaza chini huku machozi
yakimwagika kwa uchungu.
“Mchukueni huyo Malaya mumrudishe mulipo mtoa”
John
aliwaamrisha watu wake, wakamnyanyua Phidaya na kumbeba juu juu, japo
anajitahidi kujitoa mikononi mwa watu walio mbeba, huku aikiliita jina
langu kwa sauyti ya juu, ila hakuifanikiwa kujitoa mikononi mwao John
akapiga hatua hadi katika sehemu nilipo fungwa, akanitazama kwa muda,
huku macho yake yakiwa yamejaa dharau kubwa, akanitemea mate ya usoni,
akiyasindikiza kwa kofi zito lililo tua kwenye shavu langu la kushoto
“Mmmmmm Eddy, unajisikiaje?”
John
alizungumza huku akivifikisha viganja vyake, na kuvipuliza taratibu
taratibu.Akanishika sikio langu la upande wakulia, akaanza kulivuta kwa
nguvu zake zote, nikaendelea kuugulia maumivu ndani kwa ndani, sikutoa
sauti yoyote kwenye kinjwa changu
“Waooo, unajifanya komandoo usikii maumivu eheeee?”
John
alizungumza, huku akiliachia sikio langu.Akaanza kunitandika vibao
mfululizo kwenye mashavu yangu, hasira ikazidi kumiliki nafisi yangu.
“John, tumpeleke kisimani, hapo unajisumbua bure”
Victori
alitoa wazo ambalo John alilikubali, wafanyakazi wao wakanishusha
kwenye meza, majamaa wawili wakanibeba kwenye mabega yao. kama wawindaji
walio beba swala waliye muua kwenye mawindo yao.
Tukaingia
kwenye moja ya ukumbi mkubwa wenye mwanga hafifu, unao pita kwa kutumia
madirisha machache yaliyopo juu yake.Wakanibwaga chini, na kunifanya
nitoe mguno wa maumivu kutokana na kujiumiza sehemu ya paja langu,
nililo pigwa risasi Taa kubwa zenye rangi nyeupe zikawaka na kulifanya
eneo zima la ikumbu kuponekana vizuri, kuna mashimo makubwa mawili, kwa
haraka nikatabua ndio hivyo visima wanavyo vizungumzia, mabaunsa walio
kuwa wamenibeba, wakaufunga mwili wangu kwa kamba ngumu aina ya manila.
“Eddy utakufa kifo kibaya sana”
John alizungumza huku akiwa ameniinamia
“Usiombe nikatoka, kwenye mikono yeno, utajuta”
Nilizungumza kwa kujiamini sana, John akaanza kucheka kwa dharau, huku akinipiga piga mashavuni mwangu
“Eddy huwezi kutoka mikononi mwangu, nakujua wewe vizuri sana.Huwezi fanya chochote dhidi yangu.Muda wako umekwisha kaka”
“Angalia wakwako ndio utakuwa umekwisha”
John
akaanza kunipiga mateke mfululizo kwenye mbavu zangu, nikaendelea kutoa
sauti ya maumivu ila John hakunionea huruma zaidi ya kuendelea kunipiga
kwa nguvu zake zote
“Mchukueni na mukamdumbukize kwenye kisima”
John aliwaamrisha watu wake, wakanibeba, kabla hawajaondoka na mimi, Victoria akawazuia.Akapi ga hatua hadi sehemu tulipo simama
“Eddy nakupenda kaka yangu, kwaheri”
Victoria
alizungumza huku akinibusu shavuni mwangu, akawarusuhu watu kuonipeleka
kwenye kisima kilichopo kwenye huu ukumbi, kwa jinsi walivyo nifunga
kamba mwili wangu sikuweza kufanya kitu cha aina yoyote zaidia ya mwili
wangu kunyooka moja kwa moja, mithili ya mtu aliye fariki dunia.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment