Kituo cha Sheria na Haki za BInadamu (LHRC) kimetoa Ripoti ya Mtazamo
wa Hali ya Kisiasa Tanzania kwa mwaka 2016 ambayo miongoni mwa mambo
mengi yaliyoonyeshwa katika ripo hiyo ni pamoja na mikoa iliyokumbwa na
matukio mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Hapa chini ni orodha ya mikoa yenye hatari kwa wakazi wake kutokana na kukiuka haki za binadamu.
Simiyu na Kaskazini Unguja:
Mikoa
hii miwili kwa mwaka 2016 imekumbwa na changamoto kubwa katika uhuru wa
kujieleza, uhuru wa kukusanyika na haki ya kupiga kura. Lakini kwa
upande mwingine mikoa hii imepata alama za juu zaidi katika matokeo ya
mtazamo kuhusu haki za kiraia na kisiasa, hasa kwa upande wa haki ya
kuishi.
Songwe, Tabora na Shinyanga:
Mikoa hii ilipata
alama za chini zaidi ukilinganisha na mikoa mingine yote. Mikoa yote
ilikuwa na alama za chini sana kwenye uhuru ya Kukusanyika na haki ya
kuishi-mauaji na ukatili mikononi mwa vyombo vya dola. Kama serikali za
mikoa zitaendelea kuminya uhuru wa kukusanyika, kushughulikia mauaji
yanayotokana na imani za kishirikina na matukio ya kujichukulia sheria
mikononi, basi itakua ngumu kupata mwenendo chanya katika mikoa hii.
Morogoro, Arusha na Manyara:
Katika
mikoa hii kuna ongezeko kubwa la migogoro ya ardhi ambayo inaweza
kupelekea watu kujichukulia sheria mkononi au mauaji yanayofanywa na
vyombo vya dola. Migogoro hii hasa husababishwa na mvutano kati ya
wakulima na wafugaji ambapo mara nyingi hupelekea vifo vya raia.
Mbali
na mokoa hayo, kituo cha haki za binadamu pia kilitaja haki za raia
zilizoongozwa kukiukwa kwa mwaka 2016 ambazo ni pamoja na;
Haki ya Kuishi-Kujichukulia Sheria Mkononi:
Mikoa
ya Dar es Salaam na Morogoro, ambayo kwa sehemu kubwa ni mijini,
iliongoza kwa kiasi kikubwa kwenye ukiukwaji wa haki hii. Kuna haja ya
polisi na viongozi kurudisha imani ya wananchi juu yao ili kupunguza
matuko ya kujichukulia sheria mkononi.
Uhuru wa Kutoa Maoni:
Athari
ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari zitakuwa ni za muhimu sana
kufanyiwa uchambuzi kwa mwaka 2017 hasa kwa kuwa uhuru wa vyombo vya
habari umeelezwa kuwa miongoni mwa matatizo katika mikoa iliyopata alama
za chini.
Ukizingatia shinikizo ndani nan je ya nchi, itakuwa muhimu
kuangalia kama Serikali itayafanyia kazi mapendekezo ya watetezi wa haki
za 21 Matukio Makubwa yaliyotokea Mwaka 2016 Mtazamo wa Haki za Kiraia
na Kisiasa 2016 Mikoa na Haki za Kuangalia mwaka 2017 Methodologia na
Alama binadamu ya kurekebisha vipengele vya sheria hiyo vinavyominya
haki.
Uhuru wa Kukusanyika:
Tumeshuhudia zuio la mikutano
na mikusanyiko ya kisiasa kwa mwaka 2016, kitendo ambacho kimepelekea
mtazamo kwamba uhuru wa kukusanyika imeminywa. Japokuwa Jeshi la Polisi
baadae liliondoa zuio hilo, kitendo hicho kiliendelea kuathiri mtazamo
kuhusu uhuru wa kukusanyika.
Haki ya Kuishi – Mauaji na Ukatili Mikononi mwa na Vyombo vya Dola:
Matukio
ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola yamechangia kwa kiasi kikubwa
kushusha alama za haki katika mikoa mingi.
Japokuwa kumekuwa na
ongezeko la mashtaka ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola, ikiwemo
askari polisi wawili kukutwa na hatia ya mauaji hivi karibuni, kauli na
matamko mbalimbali za viongozi wa serikali ambayo yanaweza kuchochea
mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola yanaweza kuwa chanzo cha mauaji
pia.
Unaweza kupakua ripoti nzima hapa chini;
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment