Baaada
ya mazungumzo hayo,Mke huyo wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini
Rebecca Mabior amesema yeye pamoja na ujumbe wake wamelazimika kufika
nchini Tanzania kuonana na Rais Dkt Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa
Jumuia ya afrika ya Mashariki kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya
nchi ya Sudan ya Kusini.
Amemuomba
Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake wajumuia ya Afrika ya Mashariki
kulisaidia Taifa la Sudan ya Kusini kutafuta suluhisho la mgogoro
unaolikabili taifa hilo na kurejesha amani.
"Tumefarijika
kuwa hapa katika ikulu ya Tanzania na tuko hapa kumsihi Rais Dkt
Magufuli kama Mwenyekiti wa jumuia ya Afrika ya Mashariki akishirikiana
na viongozi wenzake wa jumuia hiyo kuona namna gani wanaweza kutusaidia
ili Taifa la Sudani ya Kusini liwe Taifa lenye amani,hivyo hapa
tunawakilisha vilio vya watu wa nchi yetu na kikubwa tunachokitaka ni
Amani katika nchi yetu na hiki ndio kilio chetu"
Rais
Magufuli kwa upande wake amewasihi viongozi na wananchi wa Sudan ya
Kusini kutafuta njia muafaka ya kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani
na ili kuepuka machafuko yanayosababisha mateso kwa wananchi wa Taifa
hilo.
"Mama
Rebecca hata mimi binafsi naumizwa na kile kinachoendelea katika nchi
ya Sudani ya Kusini hivyo,ningezisihi pande zote zinazotofautiana
kumaliza tofauti zao kwa amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa la
Sudani ya Kusini"
Emmanuel Buhohela
Kaimu Mwandishi wa habari Msaidizi wa Rais.
Dar es Salaam
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment