Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC
Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mabior Garang Mtoto wa Mwanzilishi
wa Taifa la Sudani Kusini Hayati John Garang De Mabior Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi
wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng Mabior Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika
ya Mashariki na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa
Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Nyandeng Garang de Mabior sambamba na
ujumbe wake akiwemo Mabior Garang ambaye ni mtoto wa Hayati John Garang
De Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam.
Picha za Mabior Garang zilizowahi kuzua utata mitandaoni.
Mabior Garang aliyekuwa Waziri wa Maji
na Umwagiliaji wa Sudan Kusini aliwahi kutikisa mitandaoni kwa picha
zake zilizozua utata huku akifukuzwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri
na Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa kile kilichosemwa kuvaa mavazi
yasiyostahili.
Mnamo Mei 6, mwaka huu, Mabior alitinga
katika kikao hicho akiwa amevaa suti nyeusi pamoja na ‘bow tie’ nyeusi
kitendo kilichopelekea kufukuzwa kwenye kikao hicho na hata alipokwenda
na kubadili tai hiyo bado hakuruhusiwa kuingia kikaoni.
Baada ya kufukuzwa Mabior Garang alivaa tai hii lakini bado hakuruhusiwa kuingia kikaoni.
Baaada ya mazungumzo hayo, Mke huyo wa
Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Mabior amesema yeye
pamoja na ujumbe wake wamelazimika kufika nchini Tanzania kuonana na
Rais Dkt Magufuli kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan
ya Kusini. Amemuomba Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake wajumuiya ya
Afrika ya Mashariki kulisaidia Taifa la Sudan ya Kusini kutafuta
suluhisho la mgogoro unaolikabili taifa hilo na kurejesha amani.
Soma taarifa kamaili kuhusu kilichozungumzwa Ikulu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment