Nay wa Mitego akiongea kwenye kipindi cha eNewz amedai mwezi uliopita ndiyo ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa mama yake lakini yeye hakuwepo hivyo aliweza kumpa zawadi za kawaida na sasa amerudi ameona ni bora amnunulie gari.
“Yeah ni kweli nimemnunulia mama yangu gari aina ya Porte japo bado hajaiona gari hiyo rasmi lakini ipo tayari kuna baadhi ya vitu namalizia then nitamkabidhi gari hiyo aina ya Porte mama yangu amekuwa akinisaidia sana na kama unavyojua mama yangu huwa ndiye anayekaa na watoto wangu muda mwingi nimeona hata nikimpa zawadi hii itakuwa inamsaidia na kurahisisha maswala ya usafiri"
Kuhusu kuchelewa kutoa zawadi hiyo, "Unajua mama yangu alizaliwa mwezi uliopita na mimi sikuwepo nilimpa baadhi ya zawadi lakini baada ya kurudi saizi nimeona nimnunulie gari kama zawadi yangu kwake ni zawadi ndogo ila kwa sasa nadhani ni kitu kikubwa kwake ila panapo majaliwa tutafanya kikubwa zaidi"
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment