Loading...

MWANA FA Adai Bifu ya Diamond na Ommy Dimpoz Inachangamsha Mziki ila Atoa Onyo


Msanii wa muziki wa hip hop, Khamisi Mwinjuma, maarufu mwana FA amedai bifu kati ya Diamond na Ommy Dimpoz ni vitu ambavyo vinahitaji kwenye muziki kwa kuwa vinachangamsha game.

Diamond na Ommy Dimpoz hivi karibuni waliingia kwenye bifu zito hali ambayo ilipelekea wawili hao kumtupiana maneno ya kashfa katika mitandao ya kijamii.

Akiongea na gazeti la Habari Leo wiki hii, Mwana FA alisema bifu la wasanii hao linachangamsha tasnia ya muziki na kusisitiza muhimu ni kudhibiti wasizuriane.

“Unajua hakuna kitu kisichokuwa na ushindani, mfano wewe upo Daily News lazima mtakuwa na washindani wenu, mnachotakiwa kufanya ninyi waandishi ni kujizuia msizuriane,” alisema FA.

“Inachangamsha muziki unapata wa kuwazungumzia, kukiwa na ushindani wa hapa na pale sifikiri kama ni kitu unachoweza kukizuia, game ikiwa rafiki sana nayo inakuwa haiwezi kuburudisha, haiwezekani mashabiki wawe wote wa wanamuziki wote hakuna kitu kama hicho,” aliongeza.

Pia rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Dume Suruali’ amedai kwa sasa bado ana mambo mengi ya kufanya katika kuendeleza muziki wake lakini pia kuendeleza familia yake pamoja na masuala ya biashara.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright KISWAGA BLOG
Back To Top