Kufuatia hatua hiyo Mheshimiwa Nassari ameahidi kushirikiana bega kwa bega na Serikali ili kuhakikisha maendeleo yanakuwa endelevu.
Mheshimiwa Nassari ametoa pongezi hizo leo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa katika majumuisho ya ziara yake ya siku 10 ya kikazi mkoani Arusha.
Mbunge huyo ambaye alilazimika kuja nchini kwa dharura akitokea masomoni nchini Uingereza ili kumuwahi Waziri Mkuu, amesema ameridhishwa na hatua za utatuzi wa migogoro ya ardhi zinazochukuliwa na Serikali.
Amesema ziara ya Waziri Mkuu mkoani Arusha, imesaidia kutibu majeraha na makovu makubwa yalitokana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana."Kama kuna kiongozi ambaye hawezi kuunga mkono jitihada hizi za kuwaletea maendeleo watu wetu, atakuwa na matatizo,” amesema.
Ameongeza kuwa kitendo cha Waziri Mkuu kuweka mikakati ya kushughulikia migogoro ya ardhi iliyodumu kwa miaka mingi ni ushahidi tosha kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwasaidia wananchi wa kawaida.
Nassari amesema mwaka 1952 wazee wa Meru walimtuma mtu kwenda Uingereza kuomba uhuru wa wananchi wa Arumeru ili waweze kujitawala na kumiliki ardhi yao kutoka kwa wakoloni.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment