Moja kati ya vipindi vigumu kwa staa wa soka wa kimataifa wa Argentina
anayeichezea FC Barcelona Lionel Messi ni kipindi hiki ambacho Argentina
haifanyi vizuri sana, Lionel Messi ambaye ni nahodha wa Argentina
aliwahi kulaumiwa na kuandikwa kuwa hajitumi timu ya taifa.
Lionel Messi pia amewahi kutuhumiwa kuwa amekuwa na sauti katika
uchaguzi wa wachezaji wa timu ya taifa mbele ya kocha wao Edgardo Bauza
madai ambayo kocha Bauza amekuwa akiyapuuzia na kukaa kimya.
Kocha Bauza ameamua kuzungumzia kuhusiana na maneno hayo “Kwa wale
wanaofikiria kuwa Lionel Messi anachagua wachezaji wa kuunda kikosi cha
timu ya taifa, sidhani kama kuna haja ya kuwajibu, kama Messi akichagua
wachezaji basi nitakuwa nje ya timu”
Kama utakuwa unakumbuka October 14 Lionel Messi alidaiwa kuhusika na
kuzuia mchezaji Mauro Icardi asiitwe timu ya taifa, kwa sababu
alimchukua mke wa mchezaji mwenzake wa Argentina na rafiki yake ambaye
amewahi kucheza nae FC Barcelona Maxi Lopez.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
Post a Comment