RAPA
maarufu nchini Marekani, Kanye West, ambaye hivi karibuni alilazwa
hospitalini baada ya kupata matatizo ya msongo wa mawazo na uchovu,
amekutana na rais mteule wa Marekani, Donald Trump jijini New York
kwenye Trump Tower ambapo ndipo yalipo makao makuu ya The Trump
Organisation, kampuni inayomiliki biashara za rais huyo mteule.
Bw Trump anasema wawili hao walizungumza kuhusu “maisha”
kabla ya kupigwa picha ya pamoja. Alisema wawili hao ni “marafiki” na
akamweleza Kanye kuwa “mtu mzuri” lakini hakusema iwapo mwanamuziki huyo
atatumbuiza wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake mwezi Januari 2017.
Kanye hakuzungumza chochote lakini akawaambia wanahabari: “Nataka tu kupigwa picha kwa sasa.”
Taarifa kutoka Marekani zinasema Bw
Trump huenda anakabiliwa na tatizo katika kutafuta wanamuziki mashuhuri
wa kutumbuiza siku ya kuapishwa kwake.
Kanye
amekuwa akipumzika na kupata nafuu kutokana na matatizo ya kiafya
aliyoyapata mwezi jana. Mwaka jana, Kanye alitangaza kwamba anakusudia
kuwania urais wa nchi hiyo ifikapo mwaka 2020, lakini hivi majuzi
alisema iwapo angepiga kura uchaguzi wa mwaka huu, basi angempigia
Donald Trump.
“Niliwaambia kwamba sikupiga kura,”
aliwaambia mashabiki San Jose, California. “Lakini sikuwaambia… iwapo
ningepiga kura, kwamba ningempigia kura Trump.”
Tangu ashinde urais, ulinzi umeimarishwa
Trump Tower, jumba ambalo rais huyo mteule amekuwa akitumia kama afisa.
Haijabainika Kanye West na Donald Trump walizungumzia nini wakati wa
mkutano huo.
Mapema Jumanne, Bw Trump alitangaza
kwamba atamteua Ofisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Exxon Mobil,
Rex Tillerson, kuwa Waziri wake wa Mambo ya Nje.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment