Dar es Salaam: KESI ambayo
imekuwa ikivuta hisia za watu wengi jijini Dar na maeneo mengine kuhusu
Salum Njwete ‘Scorpion’ ambaye anakabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa
kutumia silaha na kudaiwa kumjeruhi, Said Mrisho, ambaye kwa sasa
amepata ulemavu wa macho baada ya kutobolewa macho.
Kijana
Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu maarufu
kama Scorpion (katikati), akisaidiwa na ndugu zake (Picha na Maktaba)
Kwa mara ya kwanza, shahidi namba moja
upande mshtaki wa kesi hiyo ambaye ni Said Mrisho (aliyetobolewa macho)
ametoa ushahidi wake mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya
Ilala na kuiambia mahakama kisa chote kilichotokea hadi kutobolewa
macho.
Mshtakiwa Salum Njwete ‘Sorpion’ akifikishwa mahakamani.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa zaidi ya mashahidi sita wanatarajiwa kutoa ushahidi wao wa kumtetea Said Mrisho aliyetobolewa macho.
Baada
ya kusikiliza hoja za shahidi huyo, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya
Wilaya ya Ilala anayesikiliza kesi hiyo, Flora Haule, ameahidi kuwa
ataendelea kusikiliza mashahidi wengine wa kesi hiyo, ambapo baadaye
aliahirisha kesi hiyo na itatajwa tena Desemba 27 mwaka huu.
Kwa
upande mwingine, mshtakiwa wa kesi hiyo, Salum Njwete ‘Scorpion’
aliyefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la
Magereza, hakutakiwa kujibu chochote zaidi ya kusikiliza na kurudishwa
lupango.
Scorpion
anazidi kusota lupango toka kesi hiyo ianze huku ikivuta hisia za watu
wengi ambao wamekuwa wakijitokeza mahakamani kuisikiliza wakiwemo ndugu
zake na wale wa upande wa Said ambapo imekuwa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment