MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
"Ndio hivyo, dokta wake amesema tunaweza kumpoteza mama muda wowote kuanzia leo. Hapa nilipo nimechanganyikiwa"
Nikakata
simu, mwili mzima nikawa kama umezizima, picha ya Jonh na Sheila
zikanijia kichwani jinsi walivyo kua na furaha, nilipo waona kwenye
mgahawa.
"John nilazima ulipe kwa hili. Nikatuua kwa mkono wangu mwenyewe, ole mama yangu afe, nitakufanya kama Derick"
ENDELEA
Kila
nilicho kifikiria juu ya adhabu nitakayo mpa John, sikupata jibu la
uhakika. Nikazima kila kitu na kurudi chumbani kwetu. Nikajilaza
kitandani taratibu huku mawazo yakiendelea kuniandama. Kikubwa nikawa
ninamfikiria sana mama yangu. Sikulala hadi kunapambazuka.
"Umeamkaje baby?"
Phidaya alinisalimia mara baada ya yeye kuamka.
"Safi vipi?"
"Ahaaa poa, alafu nimeota ndoto mbaya kama nini?"
"Ndoto gani?"
"Nimeota
John amekuja hapa tulipo, akiwa na wale watu wake, akatufunga kamba,
sote wanne, kisha wakatuweka hapo sebleni. Wakamwaga mafuta ya petroli
kila sehemu, na kuwasha moto wao wakaondoka. Ndio nikastuka"
"Mmmm hakuna kitu kama hicho"
Niliamua
kumfariji Phidaya, kwani sikupenda apoteze amani asubuhi hii, ambayo
tunaendelea kujiandaa na maandalizi ya sherehe ya kuzaliwa kwa Junio
wetu.
"Hapa nilipo mapigo ya moyo yananienda mbio."
Nikamvuta karibu yangu na kumlaza kifuani mwangu, taratibu nikaanza kuzichezea nywele zake ndefu na laini.
"Tulia mke wangu"
"Eddy naogopa"
"Umaogopa nini mke wangu"
"Nahisi familia yangu, itapata shida tena. Tena hii itakua kubwa kuliko ya kwanza"
"No
baby usiyape nguvu, mawazo hayo mimi nipo. Nitahakikisha hakuna
kitakacho haribika wala mtu kunyanyua mkono wake juu ya familia yangu
nipo tayari kwa lolote hata kufa ili mradi familia yangu iishi kwa
amani"
"Kweli baby?"
"Ndio kama aliweza ile mara ya kwanza basi hii ya pili, hato weza kamwe"
Nilizungumza
huku nikiwa na jazba ya hasira, kwani hadi hapa ninavyo zidi kumfariji
mke wangu, tayari John amesha yaweka maisha ya mama yangu mashakani.
Taratibu Phidaya akaanza uchokozi wa kitandani, sikuwa na hiyana zaidi
ya kumpa haki yake anayo stahili kama mke wangu. Hadi tunamaliza kila
mmoja akawa kwenye furaha isiyo simulika, kwani wote tulifika kwa wakati
mmoja mwisho wa mechi yetu.
"Ngoja nikaandae kifungua kinywa"
"Sawa"
Phidaya
akanyanyuka na kuingia bafuni, akaoga na kutoka. Akavaa nguo alizo amua
kuvaa kwa siku hii yaleo na kwenda nje. Nikachukua simu ya mezani,
nikaziingiza namba za Blanka na kumpigia. Simu ikaita baada ya muda
ikapokelewa.
"Vipi hali ya mama?"
"Kuna mabadiliko kidogo?"
"Mazuri au mabaya?"
"Mazuri, nilimuonyesha mama picha yako ukiwa na mkeo na mwanao. Kidogo mama alianza kufungua kinywa huku akitabasamu"
"Hakusema chochote?"
"Hapana, alitabasamu tu na kutingisha kichwa kama mtu aliye furahi kwa kuiona hiyo picha"
"Poa nitakuja"
"Kwani upo wapi?"
"Nitakuambia siku nyingine. Kwaheri"
Nikakata simu, baada ya kumuona Junio akiingia chumbani huku akilia jambo lililo nistua sana.
"Mona unalia?"
"Mamy kanipiga"
Kidogo mapigo ya moyo yakanitulia.
"Kisa nini?"
"Eti hataki nimsaidie kupika chai"
"Ni hilo au kuna jengine"
"Nihilo dady"
"Mwanao ni muongo"
Phidaya aliingia huku akionekanana kukasirika.
"Amefanyaje?"
"Nimemuambia asicheze mpira ndani, likawa halinielewi. Mpaka akaipiha Tv ya ukutani ikaanguka"
"Imevunjika?"
"Hapana, haijavunjika. Tena huku nje usitoke ubaki humu humu na huyo baba yako. Sitaki kukuona huku nje sawa?"
Phidaya alizunguilmza na kutoka nje, nikamnyanyua Junio na kumtupia kitandani nilipo na kumfanya aanze kucheka na kufurahi.
"Huo uronaldo wako, uwe unaufanyia nje sawa mwangu?"
"Sawa dady, twende tukacheze nje"
Junio alizungumza huku akinivuta mkono, nikatizama saa ya ukutani inaonyesha ni saa tatu asubuhi.
"Nenda ukaningoje sebleni nioge mara moja"
"Ok dady"
Junio akatoka nikaingia bafuni na kuoga, kisha, nikavaa nguo za mazoezi na kutoka nje.
"Munaenda wapi?"
Phidaya alutuuliza baada ya kutuona tukitoka mlangoni bila ya kuaga.
"Ufukweni"
"Kifungua kinywa tayari"
"Anzeni tu sisi tunakuja"
"Eddy mbona unapenda kumuendekeza huyo mwanao, kila anacho taka unamfanyia"
Nikamfwata Phidaya na kumbusu mdomoni.
"Tunakuja baby, Shamsa yupo wapi?"
"Yupo jikoni anamalizia kupika"
"Ok tunakuja"
Tukatoka
na Junio, tukaingia kwenye lifti na kushuka hadi chini, tukitokea
gorofa ya saba, yalipo makazi yetu. Tukaelekea kwenye fukwe zilizopo
pembezoni mwa hotel hii. Kitu kilicho nishangaza ni jinsi Junio alivyo
maarufu kwa watoto wezake ambao tuliwakuta hapa ufweki. Wakaunda timu
mbili huku nami nikiwa timu pinzani na Junio. Wakanichagua kua goli kipa
na sikuwa na jinsi. Magoli ya viayu tuliyo yaweka hayakuzuia mechi
kuanza, huku golikipa wa timu ya Junio, akiwa mzee mwenye mjukuu wake
kwenye timu yangu.
Hapa
ndipo nilipo pata fursa ya kumtazama Junio vizuri, nakugundua anakipaji
kikubwa cha kucheza mpira. Mara kadhaa akawa anapiga mashuti mazito
golini mwangu, ambayo niliweza kuyanyaka vizuri. Huku wachezaji wa timu
yangu wakinisifia kwamba ninaweza kazi ya kulinda goli. Kitendo cha
kuinyaka mipira, ndivyo jinsi Junio alivyo ongeza juhudi ya kucheza na
kupiga mashuti mazito golini.
"Kumbe na wewe ni kipa mzuri?"
Mzee
wa timu ya Junio ambayo hadi sasa hivi hakuna goli alilo fungwa,
aliniuliza tulipokua tukibadilishana magoli, baada ya dakika kumi na
tano alizo tuwekea refa wetu kuisha.
"Najaribu tuu"
"Hapana, kuna kitu nimekiona ndani yako na huyo mwanao"
"Kitu gani?"
"Muna
vipaji vikubwa sana, hakikisha unamuendeleza mwanao katika fani hii,
atafanikiwa sana na atakuwa mchezaji mkubwa sana duniani"
Sauti
ya filimbi ikatustua mimi na huyu mzee, huki refa akituomba kila mmoja
akakae kwenye goli lake, tukafanya kama alivyo tuelekeza.
Mpira
ukaanza, japo kuna tifutifu jingi kwenye hii fukwe, ila Junio,
anakimbia kuliko watoto wezake ambao mara kadhaa, walikua wakianguka
anguka.
Shuti
kali alilo lipiga Junio, akiwa karibu yangu, likanipita katikati ya
miguu yangu na kwenda mbali kidogo na sehemu tunayo chezea mpira.
Nakuwafanya Junio na timu yake kushangilia ushindi wa goli hilo walilo
kua wakilitafuta kwa juhudi mara baada ya kipindi cha pili kuanza.
"Hahaaaa haaaaaa"
Nilimuona Phidaya akicheka, huku akiwa na kamera yetu. Nikatambua moja kwa moja anacheka goli, nililo fungwa na Junio.
"Junio kachukue mpira sijui umeenda wapi"
Nilimuambia
Junio aufwate mpira wake ambao yeye ndio aliuona sehemu ulipo elekea.
Junio akaongozana na wezake wawili kwenda kuutafuta.
"Unacheka nini?"
"Nakucheka wewe, ulivyo fungwa na huyo mwanao, njoo uone hili goli lilivyo ingia"
Nikamfwata Phidaya alipo, akanionyesha video aliyo rekodi, goli lililo pita katikati ya miguu yangu
"Mwanao amekupiga tobo"
"Huyu mtoto, ananguvu za miguu kama hadi ananiogopesha, skija golini"
"Ndio hivyo tumepata mchezaji, mzuri tusubirie atakaye kuja sijui atakuwaje"
"Huyo naomba awe wa kike"
"Kweli ehee"
"Au wewe unataka aweje?"
"Vyovyote Mungu atakavyo tubariki, nenda uwanjani wamesha rudi na mpira"
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment